Afisa
Masoko na Mahusiano wa Proin Promotions Ltd, Josephat Lukaza
akizungumzia Uzinduzi wa msimu wa pili wa Shindano la TMT 2015 lililopo
chini ya Kampuni ya Proin Promotions Ltd ambao pia ni wasambazaji,
wauzaji na watengenezaji wa filamu za Kitanzania. Anayeshuhudia pembeni
ni Mratibu wa Masoko wa ITV/Radio One ambao ni mmoja wa wadhamini wa
Shindano la TMT 2015.
Mratibu
wa masoko kutoka ITV/Radio One (wa pili kulia) akizungumzia juu ya
umuhimu wa wao ITV/Radio one kuwa washirika wa TMT 2015 na kuhaidi
makubwa zaidi kwa mwaka 2015.P
Mmoja
wa majaji wa shindano la TMT 2015 Yvonne Cherry au Monalisa akizungumza
mbele ya waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na shindano la
TMT 2015 lililozinduliwa rasmi leo jijini Dar Es Salaam
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2015 limezinduliwa rasmi leo huku baadhi ya vigezo vikiwa vimeboreshwa, akizungumzia hayo Meneja wa Mradi waTMT 2015, Saul
Mpock amesema kuwa "Mwaka Huu Kigezo kimojawapo ni mshiriki kuwa na
umri kuanzia miaka 16 na kuendelea huku fomu za kushiriki shindano hilo
zikipatika siku ya usaili katika mkoa husika na bila gharama yoyote"
Shindano
la Tanzania Movie Talents 2015 linaanza rasmi Kesho huku Kanda ya Ziwa
ndio itakayofungua pazia la shindano hili kwa Mwaka 2015, Shindano hili
linafanyika kikanda ambapo kanda sita za Tanzania zitafikiwa na shindano
hili.
Kwa
kanda ya Ziwa usaili utaanza tarehe 24 Aprili 2015 huku zoezi zima
likifanyika mkoani Mwanza na hatimaye zoezi kuendelea kanda ya
Kaskazini, Arusha, Kanda ya Kati, Dodoma, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,
Mbeya, Kanda ya Kusini, Mtwara na Kumalizika Kanda ya Pwani, Dar Es
Salaam.
Katika
kanda zote tano ikiwa Kanda ya Ziwa, Kaskazini, Kati, nyanda za juu
kusini na Kusini Washindi watakuwa ni watatu kutoka kila kanda ambapo
kila mshindi ataibuka na kitita cha shilingi laki tano kila mmoja huku
kanda ya Pwani itatoa washindi watano na kila mmoja kuondoka na shilingi
laki tano pia na kupelekea Washindi kuwa 20 na kuingia kwenye nyumba ya
TMT kwaajili ya Hatua ya Mchujo.
TMT
2015 itarushwa na kituo cha ITV siku ya Jumapili saa tatu usiku huku
kipindi cha kwanza kabisa cha TMT kikitarajiwa kuonekana tarehe 10 May
2015.
Shindano hili la TMT 2015 limedhaminiwa na Kampuni ya Usafirishaji ya Precision Air, I-View Studio, Global Publishers na Kituo cha ITV/Radio One ambao
ndio watakaokuwa wakirusha matangazo ya TMT 2015. TMT ikiendelea kupata
sapoti kutoka katika vituo mbalimbali za redio mikoani. Vilevile
tunatoa nafasi kwa makampuni mengine ambao wangependa kushirikiana na
TMT kwa mwaka 2015
Kauli Mbiu ya TMT 2015 ni Mpaka Kieleweke.