MAADHIMISHO ya kila mwaka ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yamefikia kilele leo katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambako kulikuwa na shughuli mbalimbali zilizofanywa na vikundi vingi, vikiongozwa na vikosi vya Ulinzi na Usalama (JWTZ).
Katika maadhimisho hayo ya miaka 51 yaliyokuwa na kauli mbiu ya Tudumishe Amani na Umoja, mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dokta Jakaya Mrisho Kikwete.

