LICHA ya kutupwa nje na Manaco
katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu huu, winga wa
Arsenal Theo Walcott anaamini klabu hiyo ndio klabu bora zaidi barani
ulaya kwa mwaka 2015.
Bila kujali kiwango cha
Barcelona au Bayern munich mwaka huu, Walcott anadai Arsenal ingeweza
kutwaa ubingwa wa ligi kuu England kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004
kama kikosi chao kisingekumbwa na majeruhi wengi.
Nyota huyo mwenye miaka 26 bado
hajawa katika kiwango chake tangu arudi kutoka kwenye majeraha na
ameanza mechi tatu tu za ligi kuu msimu huu.
“Kuna ushindani wa namba, kila
mtu anaonekana kukaza msuli na kucheza vizuri,” Walcott ameiambia Tovuti
ya Arsenal. “Imekuwa ngumu kwa watu kuingia kwenye nafasi za juu
hususani msimu huu, hakuna mtu aliyejua kama tungekuwa wa pili na
kushindania ubingwa”.
“Katika kalenda ya mwaka huu
tumekuwa timu bora barani ulaya. kwa namna kikosi kilivyo halafu kila
mmoja angekuwa fiti msimu huu tungebeba kombe. Kuna majeruhi wengi”.
Walcott amekuwa akihusishwa kujiunga na Liverpool kutokana na kukosa namba kwenye kikosi cha Arsene Wenger.