Mratibu
Mkuu wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania (Uwawata),
Julius Juju (wapili kulia) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe, ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino
na vikongwe nchini. Ripoti hiyo iliyoandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200
wa Uwawata baada ya kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa na kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa
maazimio ya kupinga mauaji hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini
katika umoja huo, Mohamed Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa
wa Dar es Salaam, Swed Omari. Makabidhiano hayo yalifanyika katika
ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akiionyesha ripoti
inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na vikongwe nchini mara
baada ya kukabidhiwa ripoti hiyo na Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba
Asili Tanzania (Uwawata), ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Ripoti
hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya kufanya
utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufanya
semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga mauaji
hayo. Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed
Masoud, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Uwawata Mkoa wa Dar es Salaam, Swed
Omari, na wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju.
Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe jijini Dar
es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akiwashukuru
viongozi wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini (Uwawata),
kwa kumkabidhi ripoti inayopinga upigaji wa ramli na mauaji ya albino na
vikongwe nchini, ofisini kwa Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.
Ripoti hiyo iliandaliwa na zaidi ya Wajumbe 200 wa Uwawata baada ya
kufanya utafiti ya mauaji ya albino katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na
kufanya semina ya hitimisho jijini Mwanza kwa kutoa maazimio ya kupinga
mauaji hayo. Wapili kulia ni Mratibu Mkuu wa Uwawata nchini, Julius Juju
na Kulia ni Mkaguzi wa Waganga nchini katika umoja huo, Mohamed Masoud.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.