Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja (Katikati)
akizungumza na waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa hafla ya
kukabidhi vifaa vya Michezo kwa klabu ya Mpira ya Lucenti,
itakayoshiriki michuano ya kanda ya Nyanda za juu kusini, itakayofanyika
Sumbawanga Mkoani Rukwa. Kushoto ni Meneja Fedha wa Benki hiyo Patrick
Kyamba na Mwenyekiti wa Klabu ya Lucent, Yusuph Liambe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja, (Katikati)
Mwenyekiti wa Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe, Mkurugenzi wa Bodi ya
Benki hiyo Margreth Kyarwenda wakiwa wameshikilia vifaa vya michezo
vilivyotolewa na Covenant Bank kwa timu hiyo itakayoshiriki michuano ya
kanda ya nyanda za juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja akimkabidhi Mwenyekiti wa
Klabu ya Lucenti, Yusuph Liambe vifaa vya michezo kwa ajili ya
maandalizi ya Timu hiyo itakayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za
juu kusini itakayofanyika Sumbawanga Mkoani Rukwa. Wanaoshuhudia ni
Meneja Fedha wa benki hiyo. Patrick Kyamba na Mkurugenzi wa Bodi
Margreth Kyarwenda.
Covenant Bank yawaita TFF, yajitolea Kuwadhamini Twiga Stars.
Dar
es Salaam, 28 Aprili 2015 . . . Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank
Sabetha mwambenja, amewaita viongozi wa Soka Nchini TFF, kwenda kujadili
namna ambavyo benki hiyo inaweza kuisaidia Timu ya Taifa ya wanawake
Twiga Stars ambayo imefuzu kushiriki Michuano ya All African Games
itakayo fanyika nchini Congo mwezi septemba.
Hayo
yametanabaishwa na Mkurugenzi huyo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya
michezo kwa timu ya Lucenti inayoshiriki michuano ya kanda ya nyanda za
juu kusini yatakayo fanyika Sumbawanga baada ya kufudhu michezo ya ligi
dalaja la tatu baada ya kuulizwa swali na waandishi waliotaka kujua ni
namna gani benki hiyo inaweza kuisaidia timu hiyo ya Taifa inayosuasua
katika maandalizi.
“Hatuna
tatizo katika kuisaidia timu ya Taifa ya Wanawake tunaweza kuwasaidia
kulingana na Mahitaji yao, ni vyema viongozi wa soka (TFF) waje tukae
tujadiliane ni Namna gani tunaweza kuisaidia timu yetu ya taifa ili
kuhakikisha inafanya vizuri katika michuano hiyo inayokuja na mingine
yote” alisema Mkurugenzi huyo.
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa timu hiyo, kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika kwenye
makao mkuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi huyo, alisema
wameamua kuvitoa ikiwa ni sehemu ya kutambua ushirikiano wao na wananchi
wa mkoa wa Ruvuma hususani wilaya ya Namtumbo.
“Tumekuwa
tukishirikiana kwa masuala mengi ya kijamii na wanachi wa Namtumbo,
tumesaidia kujenga madarasa katika shule za msingi na maabara kwa shule
za sekondari wilayani humo kuwasadia ndugu zetu kukamilisha maagizo ya
Rais yanayolenga kuinua masomo ya sayansi nchini,” alisema.
“Kwa
kutambua umuhimu wa michezo, tumeona ni vyema tuchangie pia maendeleo
ya soka katika wilaya ya Namtumbo kwa kuipa vifaa vya michezo klabu ya
Lusenti.”
Baada
ya kukabidhiwa vifaa hivyo vya Michezo, Yusuph Liambe, mwakilishi wa
Mkuu wa Wilaya Namtumbo, aliushukuru uongozi wa Benki ya Covenant kwa
kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini na kuwapa vifaa hivyo ambayo
alisema anaamini vitaleta chachu ya timu ya Lusenti kufanya vyema
katika mashindano ya soka ngazi ya kanda yatakayoanza Mei 2, mwaka huu.
Katika
mashindano hayo yanayotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
klabu ya Lusenti imepangwa Kanda ya Kusini pamoja na timu nyingine tisa
kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya na wenyeji wa kanda hiyo mkoa wa Rukwa.
“Tunaamini
vifaa hivi vitawapa nguvu wachezaji wetu kujituma na kufanya vyema
katika michuano ya kanda, hivyo vipaji vyao kuonekana na kuchukuliwa na
timu kubwa ambazo zitawapa ajira,” alisema Liambe ambaye pia ni
mwenyekiti wa klabu ya soka ya Lusenti.
Vifaa vya michezo vilivyotolewa jana na benki hiyo ni pamoja na jezi seti nne, viatu na mipira ya mazoezi.