Kiongozi
Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akizungumza na wananchi wa
kijiji cha Kintintu mara baada ya kuzindua tawi la chama hicho.
Katika
mazungumzo yake Zitto amesema ACT kinaweza kuunganisha nguvu na vyama
vingine vya upinzani ili kukiondoa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi
mkuu ujao ambapo alisema shauku kubwa ya wananchi ni kutaka kujua
msimamo wa ACT Wazalendo katika kushirikiana na vyama vingine vya siasa
ili kufanikisha malengo ya kuiondoa CCM katika madaraka.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini Singida na Kiongozi wa ACT wazalendo Zitto
Kabwe wakati akihutubia mamia ya wananchi katika uwanja wa shule ya
msingi ukombozi.
"Tumedhamiria
kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuubomoa mfumo unaonyonya wananchi.
Msimamo wetu upo wazi na tumeueleza mara kadhaa"alisema na kuongeza
“ACT-
Wazalendo tunaunga mkono juhudi zozote za kushirikiana kwa vyama na hili
linathibitishwa na jina letu Alliance na msimamo wetu kuhusu mabadiliko
ya Katiba. Kubwa tunataka ushirikiano utakaonufaisha wananchi na sio
ushirikiano wa kugawana nafasi za uongozi,” alisema Zitto.
Kiongozi
huyo wa ACT alisema chama hicho hakina tatizo na kipo tayari
kushirikiana na chama chochote kilichokuwa tayari kushirikiana nao
ikiwemo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Kiongozi
wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa Chama hicho Anna
Mghwira wakizindua tawi la chama hicho kwenye Kijiji cha Kintintu
wilayani Manyoni mkoani Singida.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo jijini humo leo.
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira, akiwahutubia wakazi wa Manyoni Mjini.
Wakazi wa Manyoni wakipiga picha na simu zao.
Zitto Kabwe akisalimiana na wakazi wa Manyoni.
Wakazi wa Mji wa Singida wakishangilia viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo wakati waa mkutano huo mjini humo leo.
Viongozi wakiimba wimbo wa taifa.
Picha kwa hisani ya Father Kidevu