Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka kushoto
akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Abiria { Terminal 11 } katika
uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar wa Abeid Amani Karume akiwa
pamoja na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar.
Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio na Msimamizi wa ujenzi wa jengo
la Abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar upande wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Nd. Yassir De Costa.
Msimamizi
wa ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar upande
wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Miundombinu na
Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De Costa akimpatiamaelezo Balozi Seif
hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa mradi huo.
Mshauri
wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka Kampuni ya
ADPI ya Nchini Ufaransa Mhandisi Guillaume Verna akifafanua hatua
zilizochukuliwa katika utaalamu utaotumika katika ujenzi wa mikonga
kwenye jengo hilo jipya la abiria.
Eneo
litakalotumika kwa huduma mbali mbali ikiwemo maduka na katika jengo
jipya la abiria linaloendelea kujengwa katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Zanzibar.
Eneo
la Nje ya jengo la Abiria litakalotumiwa na abiria wanaosafiri na
kuingia Nchini kwa kutumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume uliopo Kiembe Samaki Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Harakati
za ujenzi wa Jengo jipya la Abiria wa usafiri wa Anga katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume ulipo Kiembe Samaki Nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar zimekuwa zikiendelea kama kawaida kufuatia
marekebisho ya ujenzi wa jengo hilo utaozingatia kiwango cha Kimataifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata fursa ya
kukagua harakati za ujenzi huo unaofanywa na wahandisi wa Kampuni ya
Kimataifa ya Beijing Construction Engineering Group { GCEG } ya Nchini
Jamuhuri ya Watu wa China Chini ya Usimamizi uelekezi wa Kampuni ya ADPI
ya Nchini Ufaransa.
Msimamizi
wa ujenzi wa Mradi huo kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Nd. Yassir De
Costa alimueleza Balozi Seif kwamba ujenzi huo hivi sasa uko katika
hatua za uwezekaji paa na baadaye kuwekwa vioo.
Nd.
Costa alisema Jengo hilo kubwa litakuwa na lango kuu kwa ajili ya
abiria wote wa ndege za kimataifa na Kitaifa ambapo baadaye watajigawa
kwa mujibu wa safari za abiria hao katika huduma za ndani.
Alieleza
kwamba mizigo ya abiria itafanyiwa ukaguzi mbara mbili kabla ya
kuingizwa ndani ya ndege utaratibu ambao utathibitisha usalama wa
abiria, mizigo na eneo lote la uwanja wa ndege.
Msimamizi
huyo wa mradi wa ujenzi wa Jengo la abiria wa Serikali alifahamisha
kwamba abiria wapatao 500 watakuwa wakihudumiwa ndani ya saa moja katika
eneo la jengo hilo la abiria.
Naye
mshauri wa mradi wa ujenzi wa jengo la abiria { Terminal 11 } kutoka
Kampuni ya ADPI ya Nchini Ufaransa Mhandisi Guillaume Verna alisema
kwamba ujenzi wa Mikonga itakayohudumia ndege kubwa katika jengo hilo
imezingatiwa katika kiwango kikubwa.
Mhandisi
Guillaume alisema utafiti wa kina umefanywa katika kuona mikonga
itakayopjengwa haiathiri jengo hilo kwa mujibu wa vipimo vinavyokubalika
Kimataifa.
Mapema
Katibu Mkuu Wizara ya Maiundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma
Malik Akio alisema Serikali ya Jamuhuri ya China ambayo ndio mfadhili wa
Ujenzi huo Kupitia Benki ya Exim imeridhia kuendelea kutekelezwa kwa
mradi huo.
Dr.
Malik alisema Wizara ya Miundombinu na Mawasliano kwa kushirikiana na
wadau wa Mradi huo wanaandaa utaratibu wa kumaliza ujenzi huo kwa mujibu
wa ushauri wa Kitaalamu.
Alisema
mategemeo ya mradi wa ujenzi huo yalipangwa kukamilika mwezi Oktoba
mwaka huu lakini kutokana na kusita kwa muda ujenzi huo unatazamiwa
kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu.
Alieleza
kwamba mategemeo ya mradi wa ujenzi wa jengo hilo yalipangwa kukamikia
mwezi oktoba mwaka huu lakini kutokana na kusita kwa muda ujenzi huo
unatazamiwa kukamilika si zaidi ya mwishoni mwa mwaka huu.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alielezea
faraja yake kutokana na kuendelea kwa ujenzi wa jengo hilo ambao uko
katika hatua inayoridhisha.
Balozi
Seif aliwapongeza wahandisi wa ujenzi huo pamoja na usimamizi mahiri wa
mshauri muelekezi wa mradi huo hatua ambayo kumalizika kwake kutatoa
faraja kwa abiria wanaotumia uwanja wa ndege wa Zanzibar.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba matarajio ya abiria wanaotumia uwanja huo
wataondokana na usumbufu wa kushuka au kufuata ndege masafa marefu kwa
miguu hasa wakati wa mvua.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
20/5/2015.