Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tatu kulia), wengine ni wawakilishi kutoka balozi huo. (Picha zote na Loveness Bernard)
Waziri
wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amebeba ndoo ya
maji kichwani alipokuwa akikabidhiwa visima 33 vilivyochimbwa kwa
msaada wa Watu wa Falme za Kiarabu na Balozi wa Falme hizo.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifungua bomba la maji
kuashiria uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji katika Kata ya Olosokwani,
Loliondo wilayani Ngorongoro, juzi. Mradi huo umefadhiliwa na Serikali
ya Falme za Kiarabu (UAE) ambayo imewekeza wilayani humo. Uzinduzi huo
pia ulihudhuriwa na Balozi wa UAE nchini Tanzania, Mbarouk Nassor
Mbarouk.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akijindaa kumtwisha ndoo ya
maji mkazi wa Kata ya Olosokwani, ambako alizindua mradi mkubwa wa maji
ya visima virefu wilayani Ngorongoro, juzi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu.
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akifurahia jambo na wakazi wa
kijiji Olosokwani, baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima virefu
wilayani Ngorongoro juzi. Kushoto ni Balozi wa Falme za Kiarabu nchini
Tanzania, Mbarouk Nassor Mbarouk.
Na Loveness Bernard
Wafugaji
kutoka nchi za jirani waliovamia katika eneo la Loliondo wametakiwa
kuondoa mifugo yao mara moja ili kuliacha eneo hilo kubaki na amani.
Akizungumza
na wananchi na wafugaji wa kijiji cha Ololosokwani, Waziri wa Maliasili
na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema wakazi wa Loliondo wanauwezo wa
kutatua migogoro yao wenyewe ila wanaosababisha migogoro hiyo isiishe na
kuibuka mara kwa mara ni wageni wanaoingia katika eneo hilo na
kuchungia mifugo yao.
“Ninatoa
tahadhali kwa wageni wanaoitazama loliondo kwa jicho la husda waache
kufugia mifugo yao loliondo, kila mmoja afugie kwao ardhi ya loliondo ni
ya wana loliondo na sio wageni” alisema Nyalandu.
Alisema changamoto kubwa inayoikabili eneo hilo la Loliondo ni ongezeko la watu na mifugo wakati ardhi ikibaki kuwa ile ile.
Nyalandu
alisema kuna haja ya kuendeleza uhifadhi ili eneo la Loliondo liendelee
kustawi na wageni waendelee kuja Loliondo ambapo watachangia utalii
endelevu katika shughuli kama za utalii wa picha na uwindaji.
Akizungumzia
kuhusu miradi ya maji aliyoikabidhi kwa wananchi wa loliondo jana
kutoka kwa Balozi wa Falme za Kiarabu waliofadhiri ujenzi wa miradi hiyo
iliyogharimu sh bilioni 1.6 Waziri Nyalandu alisema hayo ni matunda ya
ushirikiano mzuri baina ya Rais Jakaya Kikwete na Mfalme wa Dubai Shekh
Makthum na Jumuiya ya falme za kiarabu.
Alisema
utekelezaji wa miradi hiyo ni ahadi ya Rais Kikwete kwa maeneo ya
wafugaji ambapo alisema azma yake ni kuona tatizo la maji katika maeneo
ya wafugaji linamazika na kuona mifugo na wafugaji wakinenepa.
Aliwataka
wananchi wa Loliondo kuitunza miradi hiyo kwa faida yao na mifugo yao
huku wakitumia muda mwingi kwa kazi za maendeleo ya loliondo.