| Haice ilivyokuwa ikionekana muda mfupi baada ya ajali |
| Lori la mchana likiwa limepinduka baada ya ajali |
Ajali hiyo imetokea jioni hii eneo
la Boma mbuzi pasua katika barabara iendayo kiwannda cha sukari TPC,imehusisha
magari mawili ambayo ni Toyota haice yenye namba za usajili SU 37299 mali ya
chuo cha mafunzo ya ufundi VETA lililogongana uso kwa uso na Tipa la mchanga
lenye namba za usajili T 202 BFT na kusababisha tipa hilo kupinduka.
Kwa mujibu wa maelezo ya askari wa barabarani aliyefika
katika eneo la tukio,aliyepata majeraha makubwa ni dereva (mwanafunzi) ambaye
jina lake halijafahamika na amewahishwa kupata matibabu.
Kwa upande wa dereva wa lori hilo bwana Victor ambaye amepata
mshituko katika mguu wake wa kulia ameelezea chanzo cha ajali hiyo kuwa ni
dereva wa haice kuingia kwa kasi katika barabara hiyo akitokea upande wa
kushoto wa barabara hiyo hivyo na kushindwa kulimudu gari na hatimaye kulifuata
lori hilo.
| Kushoto ni dereva wa Lori akiongea na askari wa barabarani ,aliyejishika kifuani ni mwalimu wa VETA aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi katika haice iliyohusika katika ajali |
| Utingo wa lori akikusanya mchanga uliomwagika baada ya ajali |
| Askari wa barabarani akijaribu kuwatuliza wananchi walitaka kumpiga mwalimu wa VETA |
“Huyu mwalimu ndiyo mwenye makosa ,huwezi kumruhusu
mwanafunzi aingize gari barabarani katika hali kama ile” alieleza bwana Hamis
Mbwana mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.
Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio gari maalum kwa ajili ya kuvuta na kuondoa magari hayo lilifika ili kuruhusu shughuli nyingine za matumizi ya barabara kuendelea.
CREDIT FUNGUKA LIVE

