Timu ya soka ya Real Madrid imetangaza kumfungashia virago vyake kocha wake mkuu Carlo Ancelotti.
Uamuzi huo umetangazwa jumatatu na Rais wa timu hiyo Florentino Perez, baada ya kushuhudia timu hiyo ikimaliza msimu vibaya.
Real
Madrid msimu huu wameshindwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Hispania al
maarufu La Liga, ubingwa ambao ulichukuliwa na FC Barcelona na pia
ilishindwa kulitetea kombe la ligi ya mabingwa barani Ulaya walilolitwaa
mwaka jana.
Rais wa timu ya Real Madrid, Florentino Perez akitangaza uamuzi wa kuachana na aliyekuwa kocha wao, Carlo Ancelotti.