https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Inashangaza? Angalia orodha ya viwanja 10 ulaya ambavyo vina wastani mzuri wa mahudhurio ya mashabiki msimu huu!

    Karibu ulaya nzima kumekua na maendeleo sana hasa katika sekta nzima ya viwanja vya kuchezea mpira wa mguu lakini gharama kubwa za tiketi na zinazidi kupanda kila msimu inasababisha idadi kubwa ya mashabiki kushindwa kumudu kila wiki na inasababisha maudhulio kushuka.
    Hata hivyo mashabiki damu wa klabu mbalimbali wamekua wakitumia hadi pesa yao ya mwisho ili kuweza kuzishudia timu zao zikiwa dimbani.
    Hebu tuangalie ni timu zipi zimekua na wastani mzuri wa maudhurio uwanjani kama ifuatavyo;
    newcastle-united
    Namba 10 imeshikiliwa na klabu ya Newcastle United toka ligi kuu ya uingereza, na idadi ya mahudhurio wastani wa mashabiki 50,402. Japokua mambo yamekua magumu sana msimu huu na
    kuwepo kwa maandamano kadhaa ya mashabiki kutomtaka mmiliki wa timu hiyo na kiwango cha timu kupanda na kushuka lakini bado wamefanikiwa kuingia katika top 10 ya viwanja ambavyo vina mashabiki wengi msimu huu.
    marseille
    Namba 9 imeshikiliwa na klabu ya Marseille kutoka pale Ufaransa ikiwa na wastani wa mashabiki elfu 51,966,Timu hiyo inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo lakini wana wastani mzuri wa mahudhurio na wameshika nafasi ya tisa ulaya nzima shukrani kwa uwanja bora kabisa wa Velodrome.
    hamburg
    Nafasi ya 8 imekamatwa na Hamburg kwa wastani wa mashabiki elfu 52,752, hawa jamaa ni kama Newcastle tu pia wao mashabiki wanabifu za chinichini na uongozi wao lakini bado mashabiki wanamiminika uwanja wa Imtech Arena kuishuhudia timu yao ikicheza.wana matumaini na kocha wao mpya Bruno Labbadia na mwamzo wake mzuri kuuendeleza na kuleta upinzani nchini ujerumani.
    arsenal2
    Nafasi ya 7 imeshikiliwa na Arsenal kwa wastani wa mashabiki elfu 59,996,ni moja ya viwanja vipya kabisa ligi kuu ya uingereza,Uwanja wa Emirates unawafanya Arsenal waendele kuwepo katika timu nne bora,japokuwa ndio timu yenye tiketi ghali zaidi lakini kila wiki mashabiki wanajazana uwanjani kuja kuiangalia timu yao japo kuna wakati wanamchukia kocha wao Arsene Wenger.
    schalke
    Schalke wapo nafas ya 6 na wastani wa mashabiki 61,553-timu hii haifanyi vizuri sana pale katika ligi ya Bundesliga wakiwa chini ya kocha Roberto Di Matteo lakini hilo haliwazuii wao kuujaza uwanja wa Veltins- Arena ambao ulijengwa mwaka 2001.
    bayern-munich
    Namba 5 ni Bayern Munich wastani wa mashabiki elfu 72,600,uwanja wa Allianz Arena ni uwanja wa tatu kwa ukubwa ujerumani na pia ni wa pili kwa maudhurio makubwa pale wanapoenda kumshuhudia Pep Guardiola Goliati akizibomoa bomoa timu nyingine.
    real-madrid2
    Real Madrid wana wastani wa mashabiki 73,227 na wanashika nafasi ya 4,uwanja huo ulipewa jina la raisi wao mashuhuri, Estadio Santiago Bernabeu, Ni uwanja bora kabisa kukaa na kumwangalia mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo pamoja na akina James Rodriguez,Karim Benzema ,Gareth Bale na Ton Kroos.
    man utd
    Namba 3 ni Manchester United na wastani wa mashabiki elfu 75,336,Hawana msimu mzuri sana mambo bado hayajatulia vizuri kama enzi za babu fergie lakini bado mashabiki wanamiminika kutoka kila upande wa duniana kuelekea pale Theatre of Dreams kushuhudia mechi za msimu.
    barcelona_0
    Barcelona wapo nafasi ya 2,labda hawajazoea nafasi ya pili kutokana na mafanikio walioyapata miaka ya hivi karibuni lakini linapokuja suala la wastani wa mashabiki hawajakamata nafasi ya kwanza,Camp Nou bado ni uwanja maridadi sana ndani ya jiji bora nani mahali perfect kuangalia mpira wa mguu.
    borussia-dortmund
    Najua huwezi amini lakini ukweli ndio huu, Namba moja imeshikiliwa na Borussia Dortmund ikiwa na wastani wa mashabiki  elfu 80,436.Ndio timu inayoongoza kwa maudhurio ya mashabiki ulaya nzima, ni miamba hii ya Bundesliga,Japokua timu hii iliyochini ya kocha ambae anamalizia ligi na kuachana nao Jurgen Klopp wamekuwa chini ya kiwango kwa msimu wote na hata nafasi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya kuwa finyu,lakini mashabiki wao hawajaacha kwenda uwanjani kuwasupport muda wote,  kama picha inavyojionyesha hapo juu utajua ni kwa nini wamekua wa kwanza.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Inashangaza? Angalia orodha ya viwanja 10 ulaya ambavyo vina wastani mzuri wa mahudhurio ya mashabiki msimu huu! Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top