Watu
takribani 12 wamearifiwa kuokolewa kutoka ndani ya nyumba zao baada ya
kuzingirwa na maji eneo la Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es salaam
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini hapa. Zeozi hili la
uokozi limefanywa na kikosi cha zima moto kutoka Ilala pamoja na vijana
wa skauti.
Licha ya zoezi hilo kupata mafanikio kwa kuokoa watu wote ambao afya
zao
zilikuwa salama vurugu pia zilijitokeza baada ya kundi moja la vijana
kupinga zoezi hilo bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi.
Chanzo: ITV Tanzania