Hali
ya taharuki imezuka katika mji wa Morogoro baada jeshi la polisi mkoa
wa Morogoro kulipua mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema na kumjeruhi mwanafunzi wa shule ya
msingi Mchikichini muda mfupi baada ya kuwachia viongozi waandamizi wa
Chadema mkoa wa Morogoro waliowekwa rumamde kwa masaa kadhaa kwa tuhuma
za kuendesha mafunzo ya ukakamavu kwa vijana.
Wakizungumza kwa uchungu wakazi wa mji wa Morogoro wamelalamikia
jeshi la polisi kulipua mabomu hovyo kwa wananchi wasio na hatia huku
wengine wakijeruhiwa na wamelitaka jeshi la polisi kutumia njia mbadala
kudhibiti wahalifu bila kuwadhuru wananchi wasio na hatia.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro
wameeleza kusikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi kutumia nguvu
kubwa ya mabomu kuwatawanya watu wachache huku wakiathiri raia wasio na
hatia ambapo katibu wa Chadema mkoa wa Morogoro Samweli Kitwika ameeleza
jinsi viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro walivyo kamatwa na kuhojiwa
na jeshi la polisi kwa masaa kadhaa na kuachiwa kwa dhamana.
kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paulo akizungumza na
waandishi wa habari amesema jeshi hilo limemshikilia mtu mmoja tu
kiongozi wa Chadema kutokana na kutoa mafunzo ya kijeshi ambapo amesema
sheria ya vyama vya siasa inazuia chama chochote kuanzisha mafunzo ya
kijeshi ndani ya chama.