Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Kulia ni Ofisa Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
Mkurugenzi
wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya
Jamii (SSRA), Ngabo Ibrahim, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari,
Dar es Salaam leo, wakati mamlaka hiyo, ilipokuwa ikitoa ufafanuzi
kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo
na Uhusiano na Uhamasishaji SSRA, Sarah Kibonde na kulia ni Ofisa
Mwandamizi Tafiti, Tathmini na Sera wa SSRA, Joseph Mutashubilwa.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye mkutano huo, wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo na Uhusiano na Uhamasishaji cha Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde, alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu kanuni No. 13 ya mafao ya wastaafu jijini leo.
MAELEZO KUHUSU KANUNI NO.13
UTANGULIZI:
Kanuni
ya Uwianishija Mafao ya Pensheni ya 2014 ina vipengele 15 ambavyo
vinalenga kuboresha mafao ya pensheni ya wanachama, kulinda na kutetea
maslai ya wanachama, kuhuisha kiwango cha uchangiaji na malipo ya
pensheni ya wanachama wa mifuko mbalimbali na kutengeneza mfumo
madhubuti ya Kisheria katika kuwianisha viwango vinavyohusiana na mafao
ya pensheni. Kipengele cha 13 kinatoa punguzo la asilimia 0.3 kwa
pensheni ya kila mwezi kutoka kwenye mafao ya mwanachama aliestaafu kwa
hiari yaani kati ya miaka 55 mpaka 59. Punguzo hili hukoma pale mstaafu
anapofika miaka 60.
Tumekuwa
tukipokea malalamiko kuhusu kanuni hiyo, lakini Tafsiri halisi ya
kipengele cha 13 cha kanuni za uwianishaji wa mafao, ni kwamba
mwanachama anayestaafu kwa hiari atapunguziwa asilimia 0.3 kwa mwezi
sawa na asilimia 3.6 kwa mwaka hadi pale atakapofika umri wa kustaafu wa
miaka 60. Hivyo si sahihi kusema kwamba kipengele hicho cha 13 cha
kanuni kinakata asilimia 18 ya mafao ya mstaafu kwa mwaka.
Badala
yake mwanachama anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 59 anakatwa
asilimia 3.6 tu kwa mwaka. Mwenye miaka 58 anakatwa jumla ya asilimia
7.2 tu kwa Mwaka, Hali kadhalika mwenye miaka 57 anakatwa jumla ya
asimilia 10.8 kwa mwaka. Kwa yule anayestaafu akiwa na miaka 55 atakatwa
jumla ya asilimia 18 katika kipindi cha miaka mitano au miezi 60.
Hata
hivyo pamoja na punguzo la asilimia 0.3 bado mstaafu wa hiari anamzidi
yule anayestaafu akiwa na miaka 60 kwa asilimia 10. Bila punguzo hilo
anayestaafu kwa hiari akiwa na miaka 55 anamzidi mwenzake wa miaka 60
kwa asilimia 28. Hii inaondoa usawa wa mafao katika hifadhi ya Jamii.
Jambo ambalo limekuwa likilalamikiwa na vyama vya wafanyakazi na
wanachama kwa ujumla.
HITIMISHO
Mamlaka
ya Udhibiti na Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii inapenda
kuwaondoa wasiwasi wanachama na kutoa wito kwa wanachama na wadau
wengine wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na kwa watanzania kwa ujumla kuunga
mkono Maboresho katika Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa lengo la kuboresha
mafao na kuifanya sekta kuwa endelevu.
Mamlaka
imeanza kufanyia kazi malalamiko ya wastaafu,iwapo kuna malalamiko
yoyote kutokana na utekelezaji wa kanuni hii basi wanachama wasisite
kuwasiliana na Mamlaka ili yapatiwe ufumbuzi mapema iwezekanavyo.
Mwisho
tunatoa shukrani zetu za dhati kwa ushirikiano mkubwa tunaopata toka
kwa vyama vya Wafanyakazi pamoja na Shirikisho lao; chama cha Waajiri;
vyombo vya habari pamoja na Serikali kwa ujumla.
Ikumbukwe kuwa:
Imetolewa na:
Kitengo cha Mahusiano na uhamasishaji
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii – SSRA
S.L.P 31846,
Simu: +255 222761683/8,
Tovuti: www.ssra.go.tz
Dar es Salaam