Kwa matokeo hayo ya kutoka uwanjani timu hizo zikiwa hazijafungana, Sunderland imefikisha pointi 38 ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi hiyo, na sasa timu ambazo mwakani hazitakuwa katika ligi kuu England, yaani zinateremka daraja ni Qeens Park Rangers ( QPR ) iliyomkiani ikiwa na pointi 30 pamoja na Burnley iliyo na pointi 30.
Baada ya kukamilika kwa mchezo huo, wachezaji, kocha pamoja na mashabiki wa Sunderland walilipuka kwa furaha baada ya kujihakikishia kubaki ligi kuu England.