Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari
wa Sekretarieti kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma
leo tarehe 22 Mei 2015.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati
Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili
ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka kanuni za
Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi kisichopungua
miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati
Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya
kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu
hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na
shughuli zao katika Chama.
Hata
hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya
kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni
za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya
Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale
wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine
watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko
ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya
wagombea utakapofika.
Taarifa
hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na
wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.
Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
22/05/2015