Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego Gutierez akifafanua jambo
alipozungumza na wahariri wa kanda ya Ziwa jana kuhusiana na jinsi
ambavyo Tigo imejipanga kuwekeza zaidi ya Sh2.6 bilioni katika kanda ya
ziwa kwa mawaka huu.
Kampuni
ya simu nza mkononi ya imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.6 kwa ajili
ya kuwekeza katika ujenzi wa minara mipya na kuboresha utoaji hudumakwa
mikoa ya kanda ya ziwa kwa mwaka 2015.
Akiongea
na waandishi wa Habari wa mkoa wa Mwanza leo, Meneja mkuu wa kampuni ya
Tigo Diego Gutierrez amesema kwamba tigo itajenga minara mipya 63,
minara hii itajumlisha minara saba yenye uwezo wa kutoa huduma ya 4G
LTE. Kanda ya Ziwa inahusisha jumla ya mikoa nane, mikoa hii ni Mwanza,
Shinyanga, Mara, Kigoma, Kagera, Tabora, Geita and Simiyu.
Teknolojia
ya 4G LTE inamaanisha kasi na uwezo mkubwa wa kutembelea intaneti na
kupakua vitu mbalimbali na pia kupata huduma isiyosumbua ya Skype. Kasi
hii pia inawezesha wateja wa Tigo kupata huduma ya video pamoja na
mikutano kwa kutumia video (video conferencing), teknolojia hii ambayo
tayari kampuni ya Tiggo wanayo, ina kasi mara tano zaidi ya ile ya 3G.
“Kwa
mwaka huu tunategemea kujenga minara mipya 63, ili kuwawezesha wakaazi
wa vijiji vyote vya mikoa hi inane ya kanda ya Ziwa kupata huduma zetu,
kwa wastani tutatumia jumla ya $ 100,000 kwa kila mnara, hii inamaanisha
kwamba tuttumia jumla ya dola 6.3 milioni kwa kanda ya Ziwa pekee,”
alisema Gutierrez.
“Kwa
hili tutakuwa tumewapatia wakaazi wa eneo la kanda ya Ziwa fursa mpya
za kijamii na kiuchumi kwa kuwapatia uwezo wa kuona yanayoendelea katika
dunia nyingine nje ya maeneo haya, kwa kutumia huduma ya intaneti
tutakuwa pia tumewapatia mageuzi ya kidijitali,” aliongeza Meneja Mkuu.
Kwa
mujibu wa Meneja Mkuu, Kanda ya Ziwa imekuwa ni eneo ambalo linafaidika
zaidi na ufadhili na shughuli mbalimbali za uwajibikaji kwa jamii (CSR)
toka kampuni ya Tigo, ambapo imekuwa ikisaidia jamii katika maeneo ya
elimu, afya, mazingira, ujasiriamali, kutengeneza ajira, sanaa na
michezo.
Katika
miaka miwili iliyopita, Tigo imewekeza wastani wa dola 2 milioni kwa
wiki katika mitandao yake hapa nchini. Uwekezaji huu ni pamoja na
kupanua wigo wa mitandao kwa kujenga minara mipya hata katika maeneo ya
vijijini, kuboresha teknolojia kwa kuleta teknolojia ya 3G ambayo
imewezesha wananchi kujipatia huduma ya data, kuwapatia mafunzo
wafanyakazi na pia kutekeleza huduma za uwajibikaji kwa jamii (CSR).
Gutierrez
pia alisema kwamba katika miezi 12 iliyopita Tigo imewezesha
upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi, ikiwa ni pamoja kuwa
kampuni ya kwanza nchini kutoa huduma za kimataifa za kifedha zikiwa
tayari zimeshawekwa katika viwango vya nchi husika, uanzishwaji wa
huduma ya Facebook kwa Kiswahili na pia kuanzisha ushirikiano na watoa
huduma wengine ili kuwawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kupitia
mitandao mbalimbali iliyopo nchini.
Meneja
Mkuu aliongeza kwamba mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuwapatia
wateja fursa ya ktoa na kuweka fedha katika akaunti mbalimbali za benki
kwa kutumia simu zao za mikononi, kuwapatia wateja gawio la faida kwa
kila robo ya mwaka katika akaunti zao za tigo pesa kutokana na salio
lililopo, huduma ya muziki kutoka Tigo ambayo inawapatia wateja uwezo wa
kupata bila kikomo muziki kutoka sehemu yeyote duniani kupitia Deezer
na teknolojia ya 4G ambayo ilizinduliwa mwezi uliopita.
Meneja mkuu wa kampuni ya Tigo, Diego Gutierez akifafanua jambo
alipoongea na wahariri wa kanda ya Ziwa jana kuhusu jinsi ambavyo Tigo
imejipanga kujenga minara mipya 63 katika kanda ya ziwa kwa mwaka huu,
wengine pichani (kutoka kushoto) ni CSR Manager Woinde Shisael, Meneja
wa Kanda ya Ziwa Ally Maswanya na Territory Manager Joseph Mutalemwa.
Meneja
Mawasiliano wa Kampuni ya Tigo, John Wanyancha akifafanua jambo kwa
wahariri wa vyombo vya habari vya kanda ya ziwa, wakati wa mkutano wao
na meneja mkuu wa kampuni ya Tigo Diego Gutierrez uliofanyika jana
jijini Mwanza.