Mkuu
wa mkoa wa Dar es slaam,Saidi Meck Sadiki(katikati) akiangalia athari
ya maji yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha hivi karibuni jijini Dar
es slaam akiwa ameambatana na wakazi wa eneo hilo la Kunduchi
Ununio.Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na DAWASA inaendelea na
zoezi la kuyaondoa maji hayo pamoja na ujenzi wa mfereji mkubwa kuelekea
baharini utakaokusanya maji kutoka Bunju na Kunduchi na kuyapeleka
bahari ya Hindi.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiki ( katikati ) akisikiliza
maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kinondoni Musa Nati wakati
akikagua utekelezaji wa zoezi la kuondoa maji katika makazi ya watu eneo
la Basihayo Tegeta.
………………………………………………………………….
Na.Aron Msigwa- MAELEZO
.Dar es Salaam.
.Dar es Salaam.
Manispaa
ya Kinondoni inaendelelea kujenga mfereji wa kudumu wenye urefu wa
Kilometa 2.1 ili kuondoa maji yaliyojaa kwenye makazi ya watu, eneo la
Basihayo -Tegeta,Bunju na Kunduchi na kuyapeleka bahari ya Hindi ikiwa
ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa hivi karibuni mara baada ya
kuwatembelea wananchi katika maeneo hayo walioathiriwa na mafuriko.
Akitembelea
maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo kujionea utekelezaji wa agizo hilo
leo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki amesema kazi ya
ujenzi wa mfereji huo utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 900
inafanyika kwa kasi inayoridhisha licha ya ugumu uliopo wa kutafuta
uelekeo wa maji hayo kutoakana na uwepo wa makazi ya watu.
Amesema
ujenzi wa mfereji huo mkubwa unakwenda sambamba na kazi ya uondoaji wa
maji ya mvua yaliyojaa katika makazi ya watu katika eneo la Basihaya
inayofanywa na Shirika la maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam huku
Manispaa ya Kinondoni chini ya usimamizi wa Muhandisi wake Baraka Mkuya
ikiendelea na uchimbaji wa mfereji wa juu na ule utakaopita chini ardhi
kuelekea baharini.
Amesema
kuwa katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa ufanisi mkubwa bila
kuathiri makazi ya watu na kulazimika kulipa fidia kwa wananchi Manispaa
hiyo inaendelea kuzungumza na baadhi ya wananchi ambao maeneo yao
yatatumika kupitisha mfereji huo waruhusu kazi hiyo iendelee huku
taratibu nyingine zikiendelea kufanyika.
Aidha
amesema kwa baadhi ya wananchi waliojenga kuta na nyumba kwenye mkondo
wa maji hususani eneo la Kunduchi Ununio na kuzuia maji kuelekea
baharini maeneo yao yatabomolewa na baadhi ya hati za viwanja kufutwa.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Kinondoni Mussa Nati akizungumza mara baada ya
kutembelea eneo hilo kushuhudia zoezi la uondoaji wa maji na ujenzi wa
mfereji huo amesema kuwa fedha zinazotumika katika kazi hiyo zinatolewa
na manispaa ya Kinondoni, na kazi hiyo itafanywa na wataalam wa Manispaa
hiyo na kufafanua kuwa kukamilika kwake kutaondoa adha ya muda mrefu ya
mafuriko waliyokuwa wanaipata wakazi hao kipindi cha mvua.
“Manispaa
ya Kinondoni tumetenga kiasi cha shilingi 900 kwa ajili ya kufungua
maji na kujenga mifereji ya kudumu inayoelekea baharini katika ili
wananchi waweze kuishi bila usumbufu wowote,na kazi hii tutaimaliza
ndani ya mwezi mmoja” Amesisitiza.
Naye
Muhandisi wa Manispaa hiyo Baraka Mkuya amesema kuwa kazi ya uondoaji
wa maji na ujenzi wa mifereji ya wazi na ile inayopita chini ya ardhi
kutokea eneo la Basihayo Tegeta na kukatisha barabara ya Bagamoyo
kuelekea bahari ya Hindi urefu wa kilometa 2.1 itakamilika ndani ya
mwezi mmoja.
Kwa
upande wao madiwani wa eneo hilo Bw.Majisafi Sharifu,Diwani wa Kata ya
Bunju (CHADEMA) na Bi.Janet Lite kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
wamesema kazi ya utekelezaji wa agizo la Rais la ujenzi wa mfereji huo
inakwenda na kueleza kuwa itakuwa faraja kwa wakazi wa kata hizo
kutokana na adha kubwa ya mafuriko ya maji waliyokua wanaipata wakati wa
msimu wa mvua.