KLABU
ya Mainz imekasirishwa mno na tabia mbaya za beki wake, Gonzalo Jara
wiki hii na haihitaji tena kuendelea kuwa naye msimu ujao.
Beki huyo wa pembeni wa zamani wa West Brom amekuwa akichezea timu hiyo ya Bundesliga tangu aondoke The Hawthorns mwaka jana.
Lakini
klabu hiyo kwa sasa ipo tayari kumuuza Jara baada ya kuonyesha utovu wa
nidhamu katika michuano ya Copa America inayoendelea nchini kwao,
Chile.
Gonzalo Jara akiangalia bega lake wakati wa mazoezi Alhamisi baada ya mambo ya aibu aliyofanya kwenye Copa America
Jara alimtia dole nyuma Edinson Cavani wakati wa mchezo dhidi ya Uruguay
Jara alizabwa kibao na mshambuliaji huyo wa PSG
Cavani alionyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kibao Jara
Kamera
zilimnasa beki huyo mwenye umri wa miaka 29 akimtia dole nyuma Edinson
Cavani, Chile ikishinda 1-0 dhidi ya Uruguay katika Robo Fainali Copa
America.
Cavani
alitolewa kwa kadi nyekundu na Jara ambaye hakuadhibiwa, baadaye
alifungiwa kutocheza sehemu yote iliyobaki kwenye mashindano hayo.
0 comments:
Post a Comment