Mabingwa
wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga wameshindwa kutamba mbele
mabingwa wa kombe la FA nchini Uganda timu ya Sports Club Villa baada ya
mabingwa hao kulazimishwa sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa
kirafiki wa kimataifa wa hisani ulioandaliwa na taasisi ya Numbani
Kwanza kwa ajili ya kuchangia watoto wanaoishi kwenye mazingira
hatarishi uliomalizika muda mfupi kwenye uwanja wa Taifa.
Winga wa Yanga na timu ya Taifa
Simon Msuva alikosa penati baada ya yeye mwenyewe Msuva kufanyiwa
madhambi na golikipa wa Sports Club Villa wakati alipopata nafasi ya
kwenda kufunga na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru ipigwe penati lakini
penati hiyo iliota mbawa baada ya Msuva kuipaisha juu.
Mchezo huo kwa upande wa Yanga
ulikuwa ni sehehemu ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya Kagame ambayo
inatarajia kuanza kutimua umbi mapema mwa mwezi Julai ikishirikisha
vilabu bingwa vya Afrika Mashariki na Kati.
Kipindi cha kwanza kilishuhudiwa
kikiwa na upinzani mkali kwa timu zote mbili kufanya mashambulizi kadhaa
kwa kupokezana lakini hakuna timu iliyoweza kuweka mpira wavuni
kutokana na washambuliaji wa timu zote mbili kushindwa kuzitumia vyema
nafasi chache zilizopatikana.
Kipindi cha pili Yanga walifanya
mabadiliko kwa kumtoa Malimi Busungu na nafai yake kuchukuliwa na Kpah
Sherman wakati Pato Ngonyani aliingia kuchukua nafasi ya Nadir Haroub
‘Cannavaro’ na Msuva akaingia kumpokea Amis Tambwe lakini mabadiliko
hayo hayakuisaidia Yanga kuweza kupata bao.
Wachezaji wapya waliosajiliwa na
Yanga Deus Kaseke akitokea Mbeya City, Geofrey Mwashiuya aliyekuwa
akikipiga Kimondo, na Malimi Busungu kutoka timu ya Mgambo JKT walipata
nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo na kuonesha viwango vizuri lakini
Geofrey Mwashiuya alionekana kukonga nyoyo za mashabiki wengi Yanga
waliojitokeza kushuhudia pambano hilo.
0 comments:
Post a Comment