Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) na Mama Maria Nyerere wakiwa katika shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri wakati wa ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri (wa tatu kulia), Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akijadiliana jambo na Mama Maria Nyerere baada ya shughuli ya kuaga mwili wa Luteni mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Marehemu Martin David Msuguri, katika ibada ya kumuaga na mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Baba yake, Jenerali mstaafu David Msuguri, Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Marehemu Martin alifariki Juni 19 mwaka huu katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua. Kulia ni Mbunge wa Mchinga (CCM), Saidi Mtanda.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati alipokwenda nyumbani hapo kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
Picha zote na John Badi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Bw. John Guido Nyerere aliyefariki Mei 9 mwaka huu, wakati alipokwenda kuhani msiba, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akitoka nje ya kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kuweka shada la maua wakati alipokwenda nyumbani hapo, kuhani msiba wa mtoto wa Baba wa taifa, Marehemu John Guido Nyerere, wilayani Butihama mkoani Mara Juni 21.2015. Picha zote na John Badi