https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    DEMBA BA KURUDISHA MAJESHI LIGI KUU ENGLAND

    DEMBA
    Wakati mshambuliaji raia wa Senegal, Demba Ba akihusishwa kurudi nchini Uingereza, World Soccer imefanya mahojiano na mshambuliaji huyo wa zamani wa Newcastle na Chelsea kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii nyumbani kwao Senegal na maisha yake ya soka nchini Uturuki.

    Mshambuliaji huyo hajakanusha taarifa za yeye kurudi kucheza tena katika ligi kuu nchini Uingereza ambapo amesisitiza bado hajamaliza biashara la ligi hiyo maarufu Ulimwenguni. Ba mwenye miaka 30 hivi sasa anakipiga katika klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki bado ana imani ipo siku atarudi tena kucheza katika ligi hii.
    Ba ambaye alizaliwa jijini Paris Ufaransa, hivi karibuni ametembelea jijini London ambako alisaidia kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasaidia watoto wasio na makazi nyumbani kwao Dakar, Senegal.
    Ba anasema, “mashabiki nchini Uturuki wana hisia na mpira na pia wanashangilia kwa nguvu zote, lakini siwezi kuficha kwamba kiwango cha soka nchini Uturuki kipo chini mno ukilinganisha na hapa (Uingereza).”

    “Kuondoka kwangu Chelsea sio la muhimu kwangu kuzungumzia lakini naamini bado mimi nin kijana, nina nafasi na uwezo wa kufanya vizuri tu hapa. Kama kuna timu zitanitaka, niko wazi kufanya kazi tena nchini Uingereza”.
    Ba atakumbukwa siku alipofunga goli akiwa Chelsea baada ya Steven Gerard kuteleza.
    Ba anasema aliondoka Chelsea, kwasababu kocha Jose Mourinho hakumuona kama ana jina la kistaa na badala yake kuwatumia Fernando Tores na veteran Samuel Eto’o.Pamoja Jose Mourinho kutokua na mpango nae lakini hilo halijawazuia wachezaji wenzake wa zamani John Terry, Banislav Ivanovic, Eden Hazard na Samuel Eto’o ambao walifika katika harambee hiyo ya usiku jijini London kuungana na Ba kuchangia pesa kwa ajili ya watoto wasio na makazi huko Senegal.
    Banislav Ivanovic amesema anamkaribisha tena Ba katika ligi huku akisema Ba alishafunga magoli mengi katika kila timu aliyoichezea na kwamba hatotumia nguvu kuthibitisha ubora wake.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DEMBA BA KURUDISHA MAJESHI LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top