https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    NEYMAR AJUTIA KWA UJINGA ALIOUFANYA UWANJANI

    neymar
    Kwa sasa hivi atakosa baadhi ya mechi baada ya kulimwa kadi nyekundu kwenye mechi ambayo wamefungwa bao moja na Colombia kwenye Copa America. Mchezaji tegemezi wa Brazil ambae ametoka kuisaidia club yake ya Barcelona kutwaa kombe la UEFA anaonekana kushindwa kuisaidia timu yake ya taifa.

    Kwenye moja ya tukio la kwenye mechi hiyo Neymar alipiga na mpira mchezaji Pablo Armero wa Colombia na baadae akaja Carlos Bacca akamsukuma Neymar na ugomvi ukatokea.
    Maamuzi yaliyotolewa ni Neymar kulimwa kadi nyekundu na Carlos Bacca kulimwa nyekundu pia. Lakini loser alikua Neymar kwasababu timu yake ilipoteza mchezo huo.
    Kwenye interview Neymar alisema anakubalia alifanya makosa na kweli hakucheza vizuri kwenye hiyo mechi pia.
    Carlos Bacca alisema kwamba anaamini Neymar kafanya hivyo kutokana na mechi kuwaendea vibaya. Ndio maana Neymar alianza kufanya ujinga kwenye mechi kwa kumpiga na mpira mchezaji wa Colombia.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NEYMAR AJUTIA KWA UJINGA ALIOUFANYA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top