Wanachama, wafuasi, mashabiki na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) mjini Sumbawanga, mkoani Rukwa wakimsindikiza Katibu
Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibroad
Slaa baada ya mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya
wakazi wa mji huo katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ndua.
Barabara za mji huo zililazimika kufungwa kwa muda na shughuli
kusimama wakati wananchi wakiwa katika shamrashamra ya kumsnikiza
kiongozi huyo ambaye yuko katika ziara ya kikazi kukagua uandikishaji
wapiga kura kwa BVR, kuhamasisha wananchi wajiandikishe kwa wingi huku
pia akikagua maandalizi ya chama kuelekea uchaguzi mkuu.