https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    IKIWA NI MWEZI WA RAMADHAN..HAWA NI WANAMICHEZO 10 BORA WAISLAM DUNIANI

    mike
    1. Marat Safin
    Mchezo: Tennis
    Miaka: 1997-2009
    Mrusi huyu mwenye hasira alipata mafanikio makubwa sana katika tennis. Safin alikuwa namba 1 duniani kwa muda mrefu, huku akishinda Grand Slams nyingi na tuzo nyingine kibao. Safin alizaliwa na kukua katika familia ya kiislam nchini Russia.

    9.Naseem Hemed
    Mchezo: Ngumi
    Miaka: 1992-2002
    Bingwa wa dunia wa uzito wa kati, Prince Naseem Hemed alialiwahi kukaa na ubingwa huo tangu 1995 hadi 2001. Ana rekodi ya kushinda kwa KO mara 31. Naseem alikuwa akimuomba Allah hadharani na kuutangaza uislam.
    1. Imran Khan
    Mchezo: Cricket
    Miaka: 1971-1992
    Alishindwa kombe la dunia 1992, ICC Hall of Fame, mchezaji bora mara 3 wa dunia. Anatajwa kuwa mchezaji bora wa Cricket wa muda wote. Aliiongoza Pakistan kutwaa ubingwa wa kwanza wa dunia 1992 wa Cricket.

    1. Bernard Hopkins
    Mchezo: Ngumi
    Miaka: 1988 hadi sasa
    Moja kati ya mabondia waliofanikiwa sana katika historia ya ngumi kwa miaka ya hivi karibuni. Ameshinda kwa KO mara 32. Bingwa wa zamani wa uzito wa kati. Aliwahi kuhukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kutokana na ukabaji akiwa na umri wa miaka 17 na baadae akajiunga na uislam. Ni bondia wa kwanza kushinda mikanda yote minne ya Uzito wa kati (WBA, WBO, WBC na Ring)
    1. Zinedine Zidane
    Mchezo: Soka
    Miaka: 1988-2006
    Mchezaji bora wa dunia mara 3, 1998 mabingwa wa kombe la dunia. Moja kati ya wanasoka adimu kuwahi kutokea ulimwenguni. Mfaransa huyo mwenye asili ya Algeria ni moja kati ya wanamichezo walioiwakilisha dini ya kiislam vizuri katika maisha yao.
    1. Mike Tyson
    Mchezo: Ngumi
    Miaka: 1981-2005
    Bingwa wa uzito wa juu wa WBC, WBA, na IBF. Tyson maarufu kama mnyama, ameshinda mapambano zaidi ya 50 huku akiwa ameshinda kwa KO mara 44. Alijiunga na Uislam mwaka 1992 alipohukumiwa kwa kosa la ubakaji. Alipotoka jela 1995 alirudi uwanjani na kushinda ubingwa wa WBC na WBA.
    1. Shaquille O’Neal
    Mchezo: Basketball
    Miaka: 1989-2011
    Bingwa mara4 wa NBA, 1990 mchezaji bora wa mwaka wa NCAA AP, MVP 3* finals, 15-time NBA All-Star, 1993 NBA Rokkie of te year. Alilelewa katika ukristo (mama) na uislam (baba), alikua sio muongeaji kuhusu dini, lakini alikuwa ni muislam wa ukweli.
    1. Hakeem Olajuwon
    Mchezo: Basketball
    Miaka: 1981-2002
    Mchezaji bora wa mashindano NCAA 1983, Mchezaji bora mara 2 wa kuzuia, 2*NBA champion, 2*NBA Finals MVP.
    Moja kati ya wachezaji hatari zaidi wa kati kuwahi kutokea NBA, mchezaji huyo raia wa Nigeria alikuwa na urefu wa futi 7. Amekua akifunga Ramadhan katika maisha yake yote.
    1. Kareem Abdul-Jabbar
    Mchezo: Basketball
    Miaka: 1966-1989
    Anaongoza kwa kufunga points nyingi zaidi katika historia ya NBA 38,387 huku akifuatiwa kwa ukaribu na Kobe Bryant 29,484. Ameshinda tuzo nyingi. Alibadili dini kutoka ukristo na kuwa muislam na kubadili jina lake la Lew Alcindor 1971.
    1. Muhammad Ali
    Mchezo: Ngumi
    Miaka: 1960-1981
    Mshindi wa medali ya dhahabu katika Olimpiki 1960 wa ubingwa wa juu. Bingwa mara3 wa uzito wa juu wa dunia. Ali ndiye nembo ya uislam katika michezo. Alikataa kushiriki katika vita kati ya taifa lake Marekani dhidi ya Vietnam kwa sababu za dini. Ali amekua msaada mkubwa kwa ukombozi wa ubaguzi wa rangi duniani. Anatajwa kuwa bondia bora kuwahi kutokea Ulimwenguni.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: IKIWA NI MWEZI WA RAMADHAN..HAWA NI WANAMICHEZO 10 BORA WAISLAM DUNIANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top