Siku hizi kumekuwa na watu na Taasisi zinazofanya harakati za kuhamasisha watu kufanya uzazi wa mpango.. wapo wanaofuata wengine hawafuati utaratibu huo kabisa.
Wapo wanaoamini kwamba wazungu wako poa sana kwenye kufuatilia ishu ya uzazi wa mpango, lakini kumbe wako wengine hawana hiyo kitu yani !!
Nimewapata hawa 11, yani kati yao mwenye watoto wachache ana watoto watatu tu !!
Angelina Jolie na Brad Pitt wote ni wakali wa action movies Hollywood.. wana watoto watatu wa kuwazaa wenyewe alafu wana watoto watatu yatima ambao waliwachukua na wanawalea kama watoto wao.
Staa wa Hip Hop ambae kwenye Ripoti ya Forbes ametajwa ndio tajiri zaidi Duniani, P Diddy ana watoto sita!
Mark Wahlberg na familia yake, watoto wake jumla wako wanne na mkewe ni huyohuyo mmoja anaitwa Rhea.
Mitt Romney aliwahi kugombea Urais wa Marekani mwaka 2012 akiwa anapambana na Obama, huyu mzee ana watoto watano na wote wa kiume.
Bondia mwenye record zake za nguvu kwenye mchezo wa ngumi, Mike Tyson.. Jamaa ana watoto nane aliozaa na wanawake saba tofauti.
Ni actor mkali pia kwenye list ya wanaowakilisha Holywood.. Kevin Costner nae ana jumla ya watoto saba.
Kati yao unaona nani kafunika kuliko wenzake mtu wangu?