Mh
January Makamba Akipokea Fomu ya Wazamini katika jiji la Mwanza kutoka
kwa Katibu wa CCM wilaya ya Ilemela Loth Olemeint. Mbunge wa Bumbuli
January Makamba ambaye anazunguuka mikoani kwa sasa kusaka wadhamini,
leo alikua katika Jiji la Mwanza huku mamia ya wanachama na wakazi wa
Mwanza walifulika katika ukumbi wa Nyanza kumsikiliza Mh January.
Makamba
ametoa ahadi kwa wakazi wa Mwanza kuwa hataka kama hatofanikiwa katika
Mchakato huu hatokua na kinyongo wala Chuki kwa atakae Teuliwa. Kwa
upande mwingine Mh January amesema kuwa anamajibu ya kiuchumi katika
Jiji la Mwanza na endapo akifanikiwa kupata nafasi hiyo atabadilisha
uchumi wa jiji la Mwanza kwa kutumia lasiri Mali za jiji hilo la Mwanza.
Picha zote na John Sambila
Msafara wa Pikipiki ukimpokea January Makamba Kuelekea Ukumbi wa Nyanza.
Mh January Makamba Akipokea Fomu ya Wazamini Kutoka kwa Katibu wa CCM wilaya ya Nyamagana Elius Mpanda.
Umati wa wakazi wa Mwanza waliojitokeza kumpokea Mh January Makamba.