Baadhi
ya Wachimbaji wadogo wadogo wakiendelea na shughuli zao za kusaka
Dhahabu katika eneo waliloachiwa wachimbaji hao eneo la Mgusu,wilayani
Geita mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Peter Malebo Mjumbe wa Kamati ya
Mgusu Miners Co. Oparative Society Limited jinsi mchanga unavyosafishwa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndug Kinana leo amehitimisha ziara yake ndani ya mkoa wa
Geita kwa kutembea kilometa 1680 kwa Gari,ametembelea Majimbo sita na
Wilaya zake sita,huku akiwa amehutubia mikutano 78,mikutano 72 ya
hadhara na mikutano 6 ya ndania.Ndugu Kinana ametembelea miradi 53 ya
Maendeleo,miradi mitano ya CCM.Kama vile haitoshi Ndgu Kinana amejizolea
Wanachama wapya 6816,Wapinzani wakiwa 640 hasa kutoka CHADEMA.
Ndugu
Kinana akiwa na msafara wake kesho anaanza ziara Mkoani Mwanza ya
Kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM
ya mwaka 2010-15,sambamba na kusikiliza matatizo ya Wananchi na
kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa dhahabu ambayo tayari
imeshapatikana baada ya kupitia hatua zote hizo kutoka kwa Mjumbe wa
Bodi ya Mgusu Miners Co Oparative Sociaty Limited Bw.Abdu Jumbe.
Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kijiji cha wachimbaji dhahabu wadogo wadogo
Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika mkutano wa hadhara
aliofanya katika kijiji hicho cha wachimbaji wadogo wa dhahabu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati
alipokagua ujenzi wa zahanati ya kata ya Nyamilyango mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na mbunge wa jimbo la Busanda
Lolensia Bukwimba wakishiriki kutandaza nyaya za umeme wa REA vijijini
katika kata ya Kasota.
Wananchi
wa kata ya Nzera wakishangilia jambo wakati katibu Mkuu wa CCM ndugu
Kinana alipozindua ofisi ya Kata hiyo,mkoani Geita leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kufukia mabomba
katika mradi wa maji wa mji wa Geita katika eneo la Kalangalala
Shilabela.
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Geita Mh. Vick Kamata akiwahutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi
Kalangalala Nyankumbu.
Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika leo, mjini Geita.
Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya
Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo.
Melfu ya
wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowahutubia
katika Uwanja wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa
katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani
Geita leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Geita Mh. Vick Kamata wakinyanyua mikono juu wakati wakikabidhi baiskeli
za viongozi wa kata wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) zilizonunuliwa
na Mbunge huyo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Nyankumbu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokea baadhi ya wafuasi wa chama cha
CHADEMA,waliokuwa wakirudisha kadi na kujiunga na chama cha CCM,kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa
Nyakumbu,mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndug Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa jimbo la Busanda Lorencia Bukwimba akihutubia katika mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipiga misumari kwenye kenchi
aliposhiriki uwekaji kenchi kwenye Nyumba ya Mganga inayojengwa katika
zahanati ya Kijiji Nyanguku, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji
wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Geita leo