Usiku
wa leo Lionel Messi atacheza mechi yake ya 100 tangu aanze kucheza
kwenye timu yake ya taifa wakati Argentina itakapokuwa inacheza dhidi ya
Jamaica kwenye michuano ya Copa America inayoendelea huko nchini Chile,
lakini karne hiyo ya mechi itafikiwa bila ya yeye kutwaa taji lolote
akiwa ndani ya uzi wa Argentina.
Mechi dhidi ya Jamaica ni mechi
ya mwisho ya Kundi B ampapo Argentina ipo pamoja na timu za Uruguay,
Paraguay na Jamaica. Mara ya mwisho Argentina kulitwaa kombe hilo
ilikuwa ni mwaka 1993 na imepita miaka 22 bila nchi hiyo kutwaa taji
jingine lolote.
Messi amepata mafanikio makubwa
yeye binafsi lakini pia akiwa na klabu yake ya Barcelona ya Hispania kwa
kuweza kuzoa tuzo ya mchezaji bora duniani mara 4, kutwaa klabu bingwa
Ulaya mara 4, ubingwa wa Hispania mara 7 na Copa del Rey mara 3.