Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakiweka jeneza la Marehemu Kamishna
Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa kwenye nyumba yake ya milele.
Mazishi hayo yamefanyika leo Juni 05, 2015 katika kijiji cha Kidia, Old
Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.
Jeneza la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa tayari limewekwa kwenye nyumba yake ya Milele.
Askofu Mstaafu Dkt. Martin Shayo wa Diyosisi ya Kasikazini akiweka akiongoza Ibada Maalum ya mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa ambaye amefariki Juni 2, 2015 katika Hospitali ya Dar Group, Jijini Dar es Salaam(kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Jeshi ka Magereza, John Casmir Minja.
Gadi
Maalum ya Maofisa wa Jeshi la Magereza wakitoa heshima kwa Marehemu
Kamishna Mkuu Mstaafu, Onel Malisa katika Gwaride la mazishi yake.
Kaburi la Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa likiwa limepambwa na mashada ya maua baada ya mazishi.
Umati wa watu waliojitokeza katika mazishi ya Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Onel Malisa.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiimba wimbo
kwenye Ibada Maalum ya kumuombea kheri Marehemu Kamishna Mkuu Mstaafu wa
Magereza, Onel Malisa baada ya shughuli za mazishi kukamilika(kulia) ni
Mchungaji Frank Machanga kutoka Jimbo la Kasikazini(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza).
