https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Msekwa:Watia nia mafisadi kukatwa

    *Ni wale wanaowania urais kupitia CCM
    WAKATI wimbi la wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania urais mwaka huu, Makamu Mwenyekiti wa CCM mstaafu, Pius Msekwa amesema wenye kashfa za rushwa watang’olewa wakati wa mchujo.

    Akizungumza na Jambo Leo, kwa njia ya simu jana kuhusu utitiri wa watangaza nia ndani ya chama hicho kama unaashiria kukua kwa demokrasia au la, Msekwa alisema CCM hakilei rushwa wala wala rushwa, hivyo watachujwa na kupata mgombea safi.
    “Chama chetu kina kanuni zake za kumpata mgombea safi wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo udiwani, ubunge na urais kwa maana lazima wapitie mchujo ambao utawang’oa wala rushwa na wale wasiohitajika,” alisema.
    Msekwa aliongeza kuwa utitiri huo wa wagombea katika nafasi hiyo kwa CCM si tatizo, kwani inaonesha ndani ya chama kuna demokrasia.
    Alifafanua kuwa wagombea wote watapita katika mchujo wa kwanza kisha kubakia watano na mchujo wa pili utafanyika na kubakisha watatu na mwisho atapatikana mmoja ambaye atapambana na wagombea wa vyama vingine.
    Msekwa ambaye ni kada maarufu wa CCM alisema kuwa Rais wa Tanzania atatoka CCM kama alivyowahi kusema Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ndiyo maana kumekuwa na utitiri wa wagombea na wote wanafahamu nafasi ya kushinda ipo chama kongwe na si kwingine.
    Msekwa ambaye amewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Tanu, aliongeza kuwa licha ya rais bora kutoka katika chama hicho, pia kujitokeza kwa wagombea lukuki kunadhihirisha demokrasia pana iliyopo ndani ya CCM na hakuna tatizo hata kama watafikia zaidi ya 40.
    Alipoulizwa kama yeye atakuwa miongoni mwa watakaotangaza nia, alisema kuwa ni kipindi cha vijana kuongoza nchi, hivyo yeye hana sababu ya kujiingiza katika kinyang’anyiro hicho.
    “Ni zamu ya vijana ingawa wananchi ndiyo wataamua, lakini hata wazee ambao wameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho nao hawatakiwi kubezwa kwani wana nafasi yao,” alisema Msekwa.
    Tayari Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula amewaonya wagombea wa urais kupitia chama hicho kuacha kutumia rushwa katika kusaka kuungwa mkono na wanachama.
    Alisema Kamati ya maadili itafuatilia nyendo za wagombea wote na kwamba ili kuona kama hawashiriki katika vitendo hivyo na kwamba wale watakaobainika hatua za kinidhamu zitachukuliwa na chama.
    Alipotakiwa kuweka wazi sifa za mgombea urais ajae, alisema kuwa vigezo hivyo ambavyo ni 13 tayari vimetajwa na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Philip Mangula.
    Mangula
    Akizungumza mjini Dodoma hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Mangula alitaja sifa za rais ajaye kuwa awe na uwezo mkubwa wa kuongoza taifa kwa kuzingatia uzoefu, uadilifu, hekima na busara na kiwango kizuri cha elimu.
    Sifa nyingine ni kuwa na upeo wa kuimarisha muungano, amani, utulivu na mshikamano wa kitaifa. Akizungumza  na waandishi wa habari, Mangula alisema mchakato unaoendelea hivi sasa ni mchakato wa urais na kuwaonya wale wote wanaoanza mchakato wa ubunge.
    Alizitaja sifa nyingine kuwa ni awe mwenye vitendo vinavyoashiria mshikamano wa kitaifa, awe na upeo mkubwa kuhusu masuala ya kimataifa, asiwe na hulka ya kidikteta, awe anaiheshimu na kulinda katiba ya nchi na utawala bora, pia asiwe ni mtu mwenye kutumia nafasi yake kujinufaisha na kujikusanyia mali.
    Mangula aliwataka wagombea wote kuacha kampeni za kupakana matope. Kuhusu mchakato wa kutafuta wadhamini kwa wagombea wa urais kwa tiketi ya CCM, alisema kwa wakati huu kila mmoja anachofanya ni kutafuta wadhamini 450 ambao wataingia katika kumbukumbu kwa ajili ya tathimini ya mgombea mtarajiwa.
    Aliziagiza kamati za maadili za wilaya kukutana mara baada ya wagombea watarajiwa kujaza majina ya wadhamini wilayani na muhtasari upelekwe mara moja makao makuu ya chama ili kamati ya maadili ya taifa itumie taarifa hizo katika kumbukumbu za kila mgombea mtarajiwa.
    Pia, aliwaonya wale wote walioanza mchakato wa kuwania ubunge kuacha kwani muda wake bado.
    “Mchakato wa kumpata mgombea wa CCM kwa ngazi ya rais umeanza, kwa ngazi ya ubunge, uwakilishi na udiwani mchakato wake bado haujaanza,” alisema Mangula.
    Alisema katika kipindi hiki cha mchakato wa uteuzi, kanuni za CCM zitatumika na kwamba ni marufuku kwa mgombea yeyote mtarajiwa au wakala wake kufanya vitendo vyovyote vinavyoonekana dhahiri ni sehemu ya kampeni za kuwania nafasi anayoitafuta.

    Rais Kikwete
    Mei 24, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alimtaja mrithi wake baada ya kuwataka wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kumchagua mgombea urais anayekubalika ndani na nje ya chama hicho na kuonya hivi karibuni kuwa yeye hana mgombea bali kura yake ni moja.

    Credit  Jambo leo 
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Msekwa:Watia nia mafisadi kukatwa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top