Baada ya kuzuiliwa na Shirikisho la
soka Afrika (CAF) kuichezea Stars dhidi ya Uganda katika mechi ya kwanza
ya kufuzu kucheza fainali za CHAN hapo Jumamosi mjini Zanzibar,
mshambuliaji Mrisho Ngassa ameibukia katika klabu yake ya zamani, Yanga
na kufanya mazoezi ili kujiweka fiti.
Kwa sasa Ngassa ni mchezaji wa Free State Stars ya Afrika Kusini baada ya kusaini mkataba wa miaka minne ya kuichezea timu hiyo.Mshambuliaji huyo amenukuliwa akisema kuwa lengo lake lilikuwa ni kuichezea Stars lakini baada ya CAF kumzuia, aliamua kufanya mazoezi ili ajiweke fiti kwa msisimko wa ligi ya Afrika ya Kusini, wakati akisubiri tiketi ya kurudi Afrika ya Kusini.
CAF ilimzuia Ngassa kwa sababu kwa sasa anahesabika kama ni mchezaji wa kulipwa baada ya kusaini kuichezea timu hiyo ya Afrika ya Kusini.
Michuano ya CHAN ni maalumu kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani na sio wanaocheza mpira wa kulipwa.
amefanya mazoezi na Yanga kwenye Uwanja wa Karume ikiwa ni maandalizi kabla hajaondoka kwenda Afrika Kusini.