“Mapokezi mliyoyafanya ni makubwa na watu waliojitokeza ni wengi sana, kama chama kinavyoelekeza kila mkoa wanahitajika wadhamini 30, kama watu wanataka kukudhamini hauwezi kuwakataa.
“Umefika wakati sasa kijiti hiki cha Urais kikabidhiwa kwa vijana ambao ni wabunifu na wataoweza kukitendea haki katika kubadilishwa taswira ya maendeleo ya nchi yetu,” amesema.
Nyalandu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini amesema, endapo atapata nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba Mwaka huu, atahakikisha anasimamia raslimali watu ambao ndio nguzo mhimu katika ujenzi wa maendeleo ya taifa.
Pia amesema, Tanzanaia kama taifa moja linao uwezo wa kuiongoza Afrika Mashariki kupitia raslimali nyingi ambazo Watanzania wamejaliwa na Mwenyezi Mungu ikiwemo madini, gesi, bunga za wanyama na misitu.
Katika Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba Mwaka huu, Nyalandu aliwataka wana CCM kuacha chuki, makundi ndani ya chama jambo ambalo litasababisha chama hicho kukosa kushika dola na kivipa nafasi vyama vya upinzani.