https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    Sentensi 20 za Zitto Kabwe, Emanuel Makaidi, Ibrahim Lipumba na James Mbatia kwenye jukwaa moja la Mdahalo

    DSC_4719
    Swali la kwanza kabisa kuulizwa kwenye Mdahalo wa Wakuu wa Vyama waliokutanishwa jana June 18 2015 Hyatt Regency Hotel DAR, lilikuwa linahusu Changamoto ambazo wao
    wanaziona TZ… Alikuwepo Prof. Ibrahim LipumbaZitto KabweJames Mbatia naEmanuel Makaidi ambapo mmoja mmoja alianza kutoa majibu ya swali hilohilo.
    Nchi za Africa huwa tunabaki kulialia sana lakini lazima uangalie wenzako Duniani kuna nini… Changamoto ya kwanza ni Katiba.. pili ni rasilimali watu, changamoto nyingine ni tofauti zilizopo kati ya watu. Kuna tatizo la umaskini, lazima pia tuwafanye Watanzania wajitambue.. Kwenye sekta ya elimu hali ya Watanzania kufikiri iko chini sana”>>> James Mbatia.
    DSC_4689
    James Mbatia, Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi
    Katika changamoto tulizonazo iko ya mama na wajawazito, katika kila watoto 100 chini ya miaka mitano, watoto 42 wana tatizo la udumavu. Changamoto ya pili ni ukosefu wa ajira na tumeanza kuona matukio kama ya panya road, watu wamepoteza matumaini kuishi kama binadamu wa karne ya 21.
    Tatizo kubwa tulilonalo ni rushwa na ufisadi, lazima tuwaweke wala rushwa wote Segerea na sio kuchukua fomu za kugombea Urais”>>> Ibrahim Lipumba.
    DSC_4772
    Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha CUF
    Ili nchi iwe sawa lazima mzawa wa Tanzania apewe nafasi ya kwanza. Changamoto nyingine ni ardhi, ardhi yetu nyingi inachukuliwa na wageni… Kingine ni Uchumi wan chi hii umedorora, ukiona fedha inapungua thamani hii ni dalili kwamba Uchumi unadorora. Changamoto nyingine ni afya, afya ya Watanzania ni mbovu. Changamoto nyingine ni elimu, hata ukienda kwenye midahalo na nchi nyingine utaona Mtanzania anapwaya” >>>Emanuel Makaidi.
    DSC_4816
    Emanuel Makaidi, Mwenyekiti wa Chama cha NLD
    Changamoto ya kwanza tuna Uchumi usiozalisha ajira, pili tuna huduma duni za kijamii ikiwemo elimu, afya na maji… Changamoto ya tatu ni rushwa na ufisadi, changamoto ya nne ni nyufa katika nchi yetu, nyufa za udini na ukabila.. Yote haya tutayatatua kwa kuweka miiko ya Viongozi, huwezi kuwa Waziri wa Kilimo na wewe ndio una zabuni ya kusambaza Mbolea, au Waziri wa Maliasili na wewe ndio una vitalu vya kuwinda” >>>Zitto Kabwe.
    DSC_4705
    Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo
    Majibu yao yako kwenye hizi sauti hapa, ukipla utawasikia wote.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: Sentensi 20 za Zitto Kabwe, Emanuel Makaidi, Ibrahim Lipumba na James Mbatia kwenye jukwaa moja la Mdahalo Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top