Watu tisa wameuwawa katika tukio la kutumia risasi kwenye kanisa la kihistoria la Wamarekani wenye asili ya Afrika huko Charleston katika jimbo Marekani la South Carolina.
Mkuu wa polisi wa mji huo Gregory Mullen amesema watu hao nane wameuwawa wakiwa ndani ya kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal jumatano jioni, ambapo mtu mmoja mwingine alifariki
Mauaji hayo yameelezwa kuwa yanatokana na chuki za kibaguzi na polisi wametoa picha za muhusika kijana mweupe zilizorekodiwa na kamera za usalama.