Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa hotuba yake ya Ufunguzi wa Mkutano wa
tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza
leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha.Mh.
Pinda awewasihi wasomi nchini pamoja na watanzania kuacha fikra ya
kusubiri kuajiriwa mara wanapomaliza vyuo badala yake wajiajiri wenyewe
ili waweze kukabiliana na changamoto za maisha.
Waziri
wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda ili aweze
kuufungua Mkutano wa tano wa Wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF) ulioanza leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa
AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
akizungumza mapema leo wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa tano wa Wadau wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ulioanza leo, kwenye ukumbi
wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, jijini Arusha. Dkt. Dau amesema, NSSF
kwa sasa imeanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali na imeshatoa mikopo kwa
wanachama wake yenye thamani ya Sh. bilioni 55.6.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimkabidhi mfano wa kadi ya Hifadhi ya wastaafu
(Hifadhi Smart Card), Bi. Kessi-Sia Mbatia (kushoto), itakayomuwezesha
Mstaafu kujipatia Fedha zake za pensheni kwa haraka, wakati wa Uzinduzi
wa huduma hiyo mpya itakayokuwa ikitolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF). Wengine pichani kutoka kulia ni Waziri wa Kazi na
Ajira, Mh. Gaudencia Kabaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg. Aboubakar Rajab pamoja
na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt.
Ramadhan Dau.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akishuhudia namna Kadi ya Wastaafu inavyofanya
kazi kupitia ATM za Selcom zitakazokuwe maeneo mbali mbali nchini ili
kuwawezesha wastaafu kujipatia Fedha zao za pensheni kwa haraka, wakati
wa Uzinduzi wa huduma hiyo mpya itakayokuwa ikitolewa na Shirika la
Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Ndg.
Aboubakar Rajab pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi
ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau.
Picha kwa hisani kubwa ya Michuzi Blog