https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIKISA JIMBONI KWAKE CHATO,WANANCHI WAIBUA SHANGWE KILA KONA YA MJI


      Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. 
    Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.

    Baadhi
    ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa 
    wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa 
    furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha 
    Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.
     Baadhi
    ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza 
    kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo 
    na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa 
    CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo 
    pichani.

     
    Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza
    kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea 
    mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi 
    wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. 
    Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra 
    shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi 
    wa 
    CCM kwa Dkt Magufuli.
     Naibu
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Luhavi akiwasalimia wachama wa CCM pamoja na 
    Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika kituo cha 
    mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.
     Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na  Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli. 

       Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji  wa Katoro mkoani Geita alipokuwa akipita njiani kuelekea wilayani Chato.Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dkt Magufuli na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.
     Mwananchi
    akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh 
    Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani 
    Geita.
    Mkuu
    wa Mkoa wa Mwanza Mh.Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato 
    jioni ya leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini 
    humo jioni ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na
    kuwashukuru. 


     Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo

     Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao. 

     
    Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa 
    kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo
    akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na 
    kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. 
    Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra 
    shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi 
    wa 
    CCM kwa Dkt Magufuli. 




     Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato



      Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi 
    CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: DKT JOHN POMBE MAGUFULI ATIKISA JIMBONI KWAKE CHATO,WANANCHI WAIBUA SHANGWE KILA KONA YA MJI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top