https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    PENATI YA NYINGI AMBAZO HAZIWEZI KUSAHAULIKA


    Asamoah-Gyan580
    Kuna beki wa Man City anaitwa Lescott, huyu jamaa ana kovu ambalo
    alilipata akiwa na mdogo sana kutokana na ajali, inawezekana kovu
    likakufanya usisahau tukio husika, pia katika soka inawezekana
    mchezaji akapata kovu la moyoni ambalo pengine anaweza asilisahau hadi
    pale mapigo ya moyo yatakaposimama…. leo ukurasa huu unakuletea
    penati ambazo ni vigumu kuzisahau kwa wachezaji husika na sisi
    mashabiki pia, karibu sana….
    Roberto Baggio v Brazili {1994}….. Inawezekana hata mke wake akifa
    ghafla leo, jamaa hapo baadae atasahau kiurahisi!!! ila kamwe hawezi
    kusahau pale ambapo aliiongoza timu yake ya taifa ya “Azuri” Kufika
    fainali ya kombe la dunia nchini Marekani, huku akifunga magoli 5
    katika michuano, Baggio alikosa penati katika fainali dhidi ya Brazil
    kutokana na presha ya mashabiki lukuki waliokuwa wanamuangalia,
    naamini penati hii utaiona kwenye DaudaTv….
    Asamoah Gyan v Uruguay {2010}….. Licha ya kwamba kwa sasa analipwa
    pesa nyingi kwa sasa pale China, achilia mbali zile alizokusanya pale
    Uarabuni na Ulaya…!!! hata umpe Pesa zimejaa Ziwa Victoria, kuna
    kitu kimoja Asamoah hawezi kusahau, sio kingine bali ni alipokosa
    penati dakika za jioni kabisa na kukatisha ndoto za mamilioni ya
    Waafrika kuona timu ya kwanza ya kiafrika ikitia maguu nusu fainali…
    ni “Moment” ambayo sio Gyan pekee hawezi kusahau bali karibu bara zima
    la Afrika, usikose kupitia DaudaTv kutazama penati hii.
    John Terry v Manchester United {2008}….. Inawezekana huyu jamaa pia
    hawezi kuusahau usiku wa pale Moscow ambapo mvua ilikuwa inanyesha,
    Terry aliteleza wakati anapiga penati na kuwapa faida Man U kutawaza
    mabingwa wa ulaya. Ni vigumu kusahau kwakuwa Chelsea kwa kipindi hiki
    walikuwa hawajawahi kuchukua ubingwa huu, japokuwa 2012 Terry
    alinyanyua “Ndoo” pale Munich ila hawezi kuusahau usiku wa pale
    Moscow, usikose kutazama DaudaTv kuona penati hii.
    David Beckham v Portugal {2004}…….  Ilikua michuano ya Euro, jamaa
    alipiga mnazi kwenye mechi ya robo fainali na kuwafanya Ureno kusonga
    mbele kwa penati 6-5, ni vigumu sana kwa David kusahau kwani mapema
    kabisa kwenye mashindani alishakosa penati kabla ya mechi hii, usikose
    kutazama DaudaTv kujikumbusha tukio hili ambalo naamini bado linaumiza
    kichwa Beckham.
    Neymar v Colombia {2012}…. Bila shaka kuna “Moment” zingine kwenye
    soka ambazo ukiziangalia kama wewe ni binadamu mwenye Bandama, basi
    lazima utacha tuu, tena sio kucheka bali “kufa-mbavu” kabisa, Neymar
    akiwa amefuga nywele zake, alianza kuruka ruka kwa mbwembwe huku
    akimuangalia Ospina, japokuwa ilikuwa mechi ya kirafiki, Neymar
    alipiga “mnazi”…. Inawezekana katika maisha yake, penati hii hawezi
    kuisahau licha ya kwamba Brazil haikupoteza katika mchezo huo, usikose
    kutazama DaudaTv.
    Amir Sayoud v Kima Aswan {2011}…. Inawezekana hii ndio penati mbovu
    kabisa kuwahi kutokea tangu soka lianzishwe, licha ya kwamba Al-Ahly
    walikuwa waongoza magoli 4, Amir alipewa kupiga penati, kwa mikogo
    jamaa akafanya kama kutisha, kilichotokea sasa…. fanya kutazama
    DaudaTv.
    Robert Pires v Manchester City {2006}…… Naamini lazima
    “utakufa-mbavu” ukitazama penati hii, kwanza Pires alipiga penati
    mbili kwenye mechi hii,  Ya kwanza alipiga vizuri na kuiandikia
    Arsenal goli la 500 pale Highbury, ila ya pili sasa ndio hawezi
    kuisahau, inawezekana alitaka kumuiga Johan Cruyff alichokifanya
    1982!!! Lengo lake lilikuwa ni kumpa pasi Henry ambaye tayari alikuwa
    kwenye box mara baada ya kipenga kupigwa, looohh!!! alichokifanya
    naamini hata yeye akiangalia hiyo “Video Clips” hawezi kuamini kama
    ndio yeye, kwa sisi watazamaji hadi kesho tunazidi kucheka maana
    hatuna namna.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: PENATI YA NYINGI AMBAZO HAZIWEZI KUSAHAULIKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top