Klabu ya Arsenal imefanikiwa kutwaa taji la Barclays Asia Trophy kwa kuifunga klabu ya Everton kwa jumla ya magoli 3-1.
Magoli ya Arsenal yamefungwa na Theo Walcott dakika 22, Santi Cazorla dakika 58 na Mesut Ozil dakika 63 wakati goli pekee la Everton lilifungwa na Ross Barkley dakika ya 76.
Mashindano ya kombe Barclays Asia Trophy yamefanyika kuanzia 15-18 July katika Uwanja wa taifa wa Singapore kwa kushirikisha timu nne ambazo ni Arsenal, Everton, Stoke City na Singapore Selection XI.
Nimekusogezea picha mtu wangu jinsi Arsenal walivyoupokea ubingwa wao.
0 comments:
Post a Comment