Mpenzi
msomaji, wiki iliyopita niliishia pale ambapo Sir Chande, kiongozi
mstaafu wa taasisi hiyo Afrika Mashariki alipokuwa akishukuru kupewa
heshima na vyombo vya kitaifa na kimataifa.
Baadhi ya
vitabu vinaonesha kwamba hakuna anayejua wanachokifanya wanachama wa
Freemasonry lakini inaaminika kuwa viongozi wakuu wa Tanzania wanajua
kila kitu.
SASA ENDELEA…
Katika
zama tulizo nazo swali la nani ni Freemason limezoeleka. Hapana shaka
kila mtu anaweza kuwa na baba, mama, babu, bibi, mjomba au binamu lakini
Freemasons ni kundi la udugu mkubwa duniani na la zamani la watu
waliojipambanua.
Kama ilivyo kundi la akina mama, kundi hili linaweza kuwa la madaktari, wafanyakazi wa benki, viwandani au walimu.
Kwa Wagiriki wa zamani, Freemasons walikuwa ni wasomi na wanafunzi wa vyuo vikuu.
Freemasons
ni watu waliojiunga pamoja kwa sababu kuna mambo au vitu wanavyotaka
kuvifanya ndani ya fikra zao. Jamaa hawa hupenda kuwa karibu mno na watu
wanaoheshimika na hueshimiana nao.
Bado
baadhi ya vitabu vinaonesha kuna mkanganyiko wa asili ya Freemasonry.
Kuna uwezekano Freemasons walishawishiwa na mashujaa wa kidini waliokuwa
kwenye kundi la kitawa la Kikristo lililoundwa mwaka 1118 kusaidia
kuwalinda waliokuwa wakienda kusali katika nchi takatifu.
Jumba
Kubwa (Grand Lodge) ambayo hata hapa kwenye ipo Posta jijini Dar ndiko
walikokuwa wakikutania. Hii ni sehemu yenye mamlaka ya kuongoza maeneo
fulani ya Freemasons.
Nchini
Marekani kuna nyumba hizi kubwa za kukutania katika Jimbo la Columbia.
Nchini Canada nako kuna majumba haya katika kila mkoa. Si hivyo tu, pia
kuna sehemu za kukutania katika kila mji na katika miji mikubwa kwa
kawaida ziko kadhaa. Nchini Marekani kuna sehemu kama hizo zipatazo
13,200.
Kwa
mujibu wa Freemasons, wenyewe ni taasisi ya kipekee inayojihusisha na
sehemu kubwa ya maisha ya kijamii nchini Marekani kwa zaidi ya miaka mia
mbili na hamsini (250) iliyopita.
Wanadai ni jumuiya yenye udugu mkubwa wa zamani na unaoendelea kuwa sehemu muhimu ya maisha binafsi ya watu na makuzi yao.
Wanasema
ni taasisi ya watu waliofungamanishwa na filosofia ya mafundisho na
uelewa wa kawaida na udugu unaowafanya watu wote kuwa sawa.Freemasons ni
watu walioamua kwamba wanapenda kujiona na kujisikia bukheri wa afya
kwao wenyewe na wengine. Hujali sana kuangalia kitu gani kitatokea siku
za usoni na hata wakati uliopita na kufanya kila wawezalo ama mtu akiwa
peke yake au na wengine. Ishu kwao ni kuufanya wakati ujao kuwa mwema
kwa kila mmoja.
Kwa
mujibu wa Mchungaji Joseph Fort Newton, mtumishi wa Mungu na mchungaji
mkuu aliyejulikana sana katika nusu ya kwanza ya karne ya 20 aliyekuwa
katika Jumba Kubwa la Iowa, kati ya mwaka 1911-1913, Freemasons si dini,
lakini imeweka msisitizo mkubwa katika Umungu Baba na kuhakikisha kuwa
udugu wa kibinadamu unafuata misingi ileile ya Umungu Baba.
Hii ikiwa
ni pamoja na wajibu wa utekelezaji wa kile kilichoitwa Golden Rule
yenye lengo la kujenga jamii moja yenye nguvu sana. Ukibahatika kukutana
na Freemasons, tarajia kuwa utakirimiwa kadiri utakavyopenda
kukirimiwa. Lengo hapa ni kukuhudumia ili uwe kama mshiriki wa Michigan,
Marekani kwenye jumba lao la kukutania la Michigan ili uwe chanzo cha
habari zinazowahusu Freemasons na wasio Freemasons kwa pamoja wa Jimbo
la Michigan na wengineo duniani.
Unawezaje
kuwa miongoni mwa Freemasons endapo tu utapata fursa ya kutupa jicho
kupita mabonde na milima hadi mwisho wa upeo kwa fikra iliyozama na
kujiona udogo wako mbele ya Mungu huku ukiwa na imani ya dini, matumaini
na ushujaa ambavyo ndiyo mzizi wa kila uadilifu.
Wakati
miti na mimea mingine maarufu ikimetemeta katika miale ya jua kwenye
maji, ikitulia kama vile mawazo ya mtu aliyependwa sana aliyekufa muda
mrefu uliopita, Freemasons kazi yao ni kumsaidia mtu anayelia kwa
huzuni.
Wakati hakuna sauti za kilio cha huzuni zinazosikika masikioni mwao, mikono yao huwa haitoi msaada bila kuwa na majibu.
Watakapoona
jambo jema katika kila imani watamsaidia mtu yeyote kuleta msaada wa
kiungu na kuiona maana tukufu za maisha bila kujali imani hiyo
inaitwaje.
Watakapoweza
kuangalia kidimbwi cha maji njiani na kuangalia ndani zaidi ya kidimbwi
hicho na kuangalia uso usio na matumaini wa mtu anayekaribia kufa na
kuona kitu kilichojaa dhambi ndipo hujitoa kusaidia.
Watakapojua
jinsi ya kusali, jinsi ya kupenda na jinsi ya kuwa na matumaini,
watakapokuwa wanajiamini wao wenyewe na kuwa na imani na wenzao na Mungu
wao huku mikononi wakiwa wameshika upanga wa ubaya, ndani ya mioyo yao
wakiimba nina furaha ya kuishi lakini naogopa kufa.
Usikose kila Jumatano kwenye Gazeti hili la Risasi Mchanganyiko. Kwa maoni tuwasiliane kwa namba hiyo hapo juu
0 comments:
Post a Comment