Hakuna mzaha kwa hili!, bosi wa Chelsea, Jose Mourinho anamtaka kwa nguvu zote John Stones katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mourinho anamuona mlinzi huyo wa Everton kama mrithi wa nahodha wa muda mrefu wa The Blues, John Terry na yuko tayari kuvunja benki ili kupata huduma yake.
Kocha wa Everton, Roberto Martinez anaweka ngumu kuuza ‘chombo’ hicho cha maana, lakini Mourinho amekomaa naye.
The Guardian wameripoti kwamba Chelsea wapo tayari kuvunja rekodi ya usajili kwa beki huyo wa England ili kumshawishi Martinez.
Mwaka 2002, Rio Ferdinand alisajiliwa na Manchester United kutoka Leeds kwa dau la paundi milioni 30 na mpaka sasa anabakia kuwa mlinzi ghali zaidi katika historia ya soka la England.
Everton tayari wamekataa ofa ya paundi milioni 20 na Chelsea wanajaribu kuwashawishi kwa paundi milioni 26, wakikataa, Mourinho anaongeza mzigo mwingine mpaka kieleweke
0 comments:
Post a Comment