Kuna nchi ambazo sehemu ya kitega uchumi kwao ni kwenye soka!! ukiachia miundombinu ya barabara na majengo mazuri,zipo nchi ambazo huthamini zaidi mpira wa miguu na zimejikuta zikiwekeza zaidi katika mchezo huo.
Moja ya sababu zinazofanya nchi za Ulaya kufanya vizuri katika michezo ni pamoja na miundombinu mizuri inayowawezesha kuwa na mazingira mazuri ya kufanya vizuri.
Leo nimekusogezea hivi viwanja 10 vilivyojengwa kwa gharama zaidi:-
1. Uwanja wa Metlife stadium upo katika mji wa East Rutherford, Marekani, una uwezo wa kuchukua mashabiki 80,000-uligharimu kiasi cha dola bilioni 1.6
2. Uwanja wa Yankees Stadium upo New York, ulijengwa mwaka 2009 na kugharimu kiasi cha dola bilioni 1.50
3. Uwanja wa Olympic Stadium upo Montreal, Canada, ulijengwa mwaka 2004 na kugharimu kiasi cha dola bilioni 1.47
4. Uwanja wa AT&T Stadium, upo Texas-ilijengwa mwaka 2009 na kugharimu kiasi cha dola bilioni 1.4
5. Uwanja wa Wembley Stadium upo London Uingereza-umegharimu kiasi cha dola bilioni 1.35
6. Uwanja wa Madson Square Garden upo New York, Marekani-umegharimu kiasi cha dola bilioni 1.1
7. Uwanja wa Nissan Stadium upo katika mji wa Yokohama, Japan-umegharimu kiasi cha dola milioni 990
8. Uwanja wa Stade Stadium de France, umetumia kiasi cha dola milioni 974 na una uwezo wa kubeba watu 80,000
9. Uwanja wa Rogers Center upo Toronto, Canada-ulijengwa mwaka 2005 na kugharimu kiasi cha dola milioni 930
Uwanja wa Jamsil Olympic stadium upo Korea Kusini, ulijengwa mwaka 1988 na kugharimu kiasi cha dola milioni 923
0 comments:
Post a Comment