Matarajio ya mashabiki wa timu mbalimbali za soka duniani ikitokea wachezaji wamesajiliwa na timu zao kwa ada kubwa ya uhamisho, wanasubiri kuona wachezaji hao wanafanya vizuri katika timu mapema.. na hali hiyo sio kwa mashabikio peke yao ila hata Kocha wa Manchester United Louis van Gaal.
Licha ya ushindi wa goli 3-1 walioupata Man United dhidi ya San Jose Earthquakes,kocha wa Man United Louis Van Gaal amelalamikia kiwango kibovu alichokionesha kiungo wa kijerumani Bastian Schweinsteiger ambaye amesajiliwa msimu huu akitokeaFC Bayern Munich ya Ujerumani kwa ada ya uhamisho inayokadiriwa kufikia pound milioni 15.
“Mchezaji anaweza kucheza vibaya kama amefanya mazoezi kwa siku tatu hadi sita, lakini anaweza kumudu kucheza kwa dakika 45. Schweinsteiger alicheza vibaya, nafikiri mechi ya kwanza alicheza vizuri ila kwa hii amecheza vibaya”>>>Louis van Gaal
0 comments:
Post a Comment