https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    “HATA LIONEL MESSI ANGEPATA WAKATI MGUMU KUVAA VIATU VYAKE”

    CKfhCE5UAAA_Ixn
    James Milner amesisitiza kwamba hakuna mchezaji yeyote katika sayari hii anayeweza kurithi viatu vya nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard katika dimba la Anfield.
    Milner, 29, ambaye amejiunga na Liverpool majira haya ya kiangazi akiwa mchezaji huru amesema hata Mwanasoka bora mara nne wa Dunia, Lionel Messi hawezi kurithi mikoba ya Gerrard.
    “Sidhani kama kuna mtu yeyote kwenye sayari hii ambaye anaweza kuvaa viatu vya Gerrard Anfield na kufikia mambo yote aliyoyafanya kwa miaka yote aliyodumu.  Sisi kama timu tunahitaji kurithi jitihada zake”. Amewaambia ABC.
    “Kwa yale aliyofanya Stevie, hata Messi (Lionel) angepata wakati mgumu kuvaa viatu vyake”. Ameongeza Milner ambaye alicheza pamoja na Gerrard wakiitumikia timu ya Taifa ya England.
    “Yale aliyofanya ndani na nje ya uwanjani, kama mchezaji, kama nahodha wa timu, kama mtu wa kawaida, hakika yanashangaza. Ni ngumu kurithi, lakini nina uhakika kama timu tunaweza”.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: “HATA LIONEL MESSI ANGEPATA WAKATI MGUMU KUVAA VIATU VYAKE” Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top