Timu ya taifa ya wanawake ya Marekani imetwaa kombe la dunia kwa upande wa wanawake baada ya kuichakaza Japan kwa goli 5-2 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jana usiku nchini Canada.
Magoli matatu (hat-trick) ya Carl Lloyd ndani ya kipindi cha kwanza yalitosha kabisa kuiangamiza Japan ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo. Magoli mengine ya Marekani yalifungwa na Lauren Holiday na Tobin Heath alifunga goli la tano na la mwisho kwenye fainali ya jana.
Yuki Ogimi alifunga goli la kwanza kwa upande wa Japan wakati Julie Johnston alijifunga na kuifanya Japan kupata magoli mawili.
Fainali ya jana ilikuwa ni ya marudio ambapo mwaka 2011 timu hizo zilikutana kwenye hatua kama hiyo na Japan wakafanikiwa kutwaa kombe kwa kuifunga timu ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment