https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania


.

.

.
  • Latest News

    .

    MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA AMESEMA HAYA…

    Donald NgomaMshambuliaji mpya wa Yanga Donald Ngoma aliyesajiliwa akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, amesema amefurahi kujiunga na klabu hiyo ya Jangwani na kuongeza kuwa, kucheza kwenye klabu hiyo sio kitu rahisi kwasababu timu hiyo ni moja kati ya timu kubwa barani Afrika na atajitahidi kufanya kile ambacho mashabiki wanatarajia kutoka kwake.
    “Nina furaha kujiunga na Yanga, ni miongoni mwa klabu kubwa Afrika ina uongozi bora, mashabiki bora, waalimu bora pia na kikosi bora. Hatukutegemea (yeye na Zuttah) kama tungepata mapokezi kama haya kutoka kwa mashabiki tumeshangazwa sana na jinsi mashabiki walivyo wengi na wanavyoipenda timu yao”, amesema Ngoma
    Najua kuchezea klabu kubwa kama hii kuna presha kubwa sana lakini naamini nitaishinda hiyo presha na kufanya kile mashabiki wanachotarajia kutoka kwangu, siwezi ahidi chochote zaidi ya kusema kazi yangu uwanjani ndio itatoa majibu”, alisema Mzimbabwe huyo.
    Donald Ngoma Dombo anaondoka leo kurudi kwao kwa ajili ya kujiandaa rasmi ili kuja kuitumikia Yanga ambapo atarudi Jumapili na siku ya Jumatatu ataanza mazoezi kujiandaa na michuano ya Kagame.
    https://play.google.com/store/apps/details?id=com.blog.ya.watanzania

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MSHAMBULIAJI MPYA WA YANGA AMESEMA HAYA… Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top