Eden Hazard akionesha mambo yake
Mabingwa wa kandanda England, Chelsea wameanza vibaya ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani baada ya kupokea kipigo kikali cha 4-2kutoka kwa New York Red Bulls.
Mabao ya Chelsea yamefungwa Loic Remy (26) na Eden Hazard (75).
Waliocheka na nyavu kwa upande wa Red Bulls ni Franklin Castellanos (51), Tyler Adams (67) na Sean Davis (73, 78).
Hata hivyo Jose Mourinho amesema kikosi chake kimefanya mazoezi kwa wiki moja tu, hivyo wachezaji hawana kasi kwasababu wamechoka.
Straika wa Chelsea, Diego Costa akijaribu kumfunga Golikipa Santiago Castano
Mlinzi wa Chelsea, Branislav Ivanovic, akichuana na mchezaji wa New York Red Bulls
Kiungo wa Chelsea, Ramires akipambana na kiungo wa New York Red Bulls, Davis
Victor Moses, ambaye amerejea kutokea Stoke ambako alikuwa anacheza kwa mkopo akimtoka Daniel Bedoya
Oscar akijaribu kumiliki gozi
Ivanovic akisafiri hewani kugonga kichwa
0 comments:
Post a Comment