Wakala wa Robin van Persie amekanusha taarifa zilizo zagaa kuwa Van Persie ameshakubaliana na klabu ya Fenerbahce lakini ameweka wazi kuwa, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anarejea Carrington (uwanja wa mazoezi wa Man United) kujiunga na kikosi cha United kuanza mazoezi baada ya mapumziko ya mwishoni mwa ligi.
Inaeleweka kuwa, mpaka sasa hakuna dili lolote lililofanyika kati ya Manchester United na klabu hiyo ya Uturuki na vyanzo vya karibu kutoka kwa Van Persie vinasisitiza kwamba, mchezaji huyo anataka kuendelea kusalia Old Trafford kwa muda wote uliobakia kwenye mkataba wake.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 amepanga kukutana na kocha Louis van Gaal ili kufanya mazungumzo kujua nafasi yake kwenye kikosi hicho.
Alipoulizwa kwamba Van Prsie huenda akaondoka na anatafuta timu yenye uwezo wa kulipa pauini milioni 12 kufidia mkataba wake wa miezi 12 iliobaki kwenye mkataba wake, Kees Voss alisema: “Kama Robin angekuwa amepata timu mpya tungeshaitangaza. Na kwasasa nipo Uholanzi”.
“Naweza sema kwamba Robin atajiunga na Manchester United kwa ajili ya mazoezi ya kwanza kwa ajili ya msimu ujao”.
Kilakitu kitategemea kama United watamsajili mshambuliaji mwingine, mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Napoli Gonzalo Higuai na Edinson Cavan ambaye ni mkali mwingine wa timu ya taifa ya Uruguay na klabu ya PSG ndio miongoni mwa washambuliaji wanapewa nafasi kubwa ya kusajiliwa na Mashetani Wekundu.
Kama Van Persie atakuwa ni mshambuliaji chaguo la tatu, atalazimika kuikacha timu hiyo kwasababu nataka kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza ili aweze kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Uholanzi kitakachoshiriki michuano ya Euro mwaka 2016.
United tayari wako sokoni kutafuta mshambuliaji wa kuchukua nafasi iliyoachwa na Radamel Falcao na wanaweza wakamuuza Javier Hernandez ‘Chicharito’ na kumtoa kwa mkopo James Wilson.
0 comments:
Post a Comment