Yanga wameshindwa kutamba kwenye
uwanja wa nyumbani baada ya kubanjuliwa na vigogo vya Kenya timu ya Gor
Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Kagame Cup uliopigwa leo
jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga walitangulia kupata goli
dakika ya nne kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao mpya
Donald Ngoma walie msajili kutoka klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe
lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani Haruna Shakava aliisawazishia
Gor Mahia goli hilo dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza na timu hizo
kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Mshambuliaji wa Yanga Donald
Ngoma alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza baada ya
kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Gor Mahia.
Michael Olunga aliifungia Gor
Mahia goli la pili dakika ya 45 katika kipindi cha pili na kuipa ushindi
timu yake dhidi ya Yanga, mabingwa wa Tanzania bara (Yanga)
walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini mambo yalikuwa magumu
kwa upande wao.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikosa
mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Gor Mahia kuunawa mpira kwenye eneo
la hatari wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa shambulizi lililofanywa
na Yanga wakati wakilisakama lango la Gor Mahia wakitafuta goli la
kusawazisha.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha
wa Yanga Hans van der Pluijm kwa kuwaingiza wachezaji Kpah Sherman
akichukua nafasi ya Simon Msuva, Deusi Kaseke akampisha Salumu Telela
wakati Joseph Zutah akaingia kumpokea Juma Abdul lakini mabadiliko hayo
hayakuzaa matunda.
0 comments:
Post a Comment