Sherehe za kutimiza michezo 100 kwa Jose Mourinho katika dimba la Stamford bridge ziliharibiwa na kichapo kutoka kwa Crystal Palace. Kilikua kichapo cha kwanza kwa Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani wa Stamford bridge tangu April 2014 na kichapo cha pili kwa Mourinho katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge katika michezo 100 aliyoitimiza jana.
Katika mkutano na waandishi wa habari Mourinho alisema “Walikuja na kila kitu walichokua nacho, timu yao ilikua imejianda, wachezaji wao walikua wamejiandaa, walikuja na morali ya ajabu. Walikua na bahati lakini walistahili hiyo bahati na waliipigania”
“Nahisi tulistahili zaidi. Sisemi kwamba tulistahili kushinda sababu sio kweli, ila tulistahili”
Mourinho alilaumu baadhi ya wachezaji wake kwa kuonesha kiwango cha chini katika mechi hiyo ili kuweza kutetea ubingwa wao.
“Golikipa na mabeki wangu wawili wa kati walikua katika kiwango kizuri sana, tulitengeneza nafasi nyingi ila kuna baadhi ya wachezaji hawakua kwenye mchezo. Katika hatua hii unavyokua na mpinzani mzuri aliyejipanga na ana morali ya hali ya juu, hana cha kupoteza unahitaji watu wafanye kazi. Siwezi sema nilikua na wachezaji 11 waliokua wanacheza kwa wakati mmoja” Mourinho alisema.
“Wachezaji wawili au watatu walicheza chini ya kiwango na nina jilaumu kwa kumuacha mmoja wao acheze kwa dakika 90. ”
Ushindi wa Manchester City yenye point 12 unafanya kue na tofauti ya point 8 kati yao na Chelsea yenye point 4. Lakini Mourinho amesema hilo haliwatoi katika mbio za ubingwa.
“Tunatofauti ya point 8 na anaeongoza ligi na ingekua kwenye ligi nyingine ningesema tushapoteza ubingwa sababu katika hizo ligi inakua ni vigumu kwa timu za juu kupoteza point nyingi hivyo. Ila katika ligi ya uingereza sisemi kama ligi imeisha. ”
“Ukweli ni kwamba tumeanza ligi vibaya, point nne katika michezo minne ni mwanzo mbaya sana”
0 comments:
Post a Comment